Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Yusufu Masauni akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba katika kikao cha kufanya tathimini ya mauaji nchini.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
ZAIDI ya watu 150 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Nchini kwa kipindi cha ndani ya mwezi mmoja kuanzia Januari Mosi hadi 31 mwaka huu kutokana na tuhuma za mauaji yaliyotokea katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Haya yamesemwa leo jijini Dodoma Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Yusufu Masauni katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba katika kikao na Uongozi wa juu hilo kujadili kadhia ya mauaji yanayoendelea nchini ili kupata ufumbuzi wakudumu.
Waziri huyo amesema lengo la kikao hicho ni kujiridhisha na kufanya tathmini kujua nini kifanyike ambapo amepokea taarifa ya Mwezi mmoja kuhusiana na matukio hayo.
Ametaja Mikoa vinara ya matukio ya mauaji ni Kagera, Dodoma,Mara,Tabora,Kigoma,Ruvuma na Songwe pamoja na hayo Waziri Masauni ameunda Kamati ya kuishauri Serikali nini kifanyike ili kupata suluhisho lakudumu la matatizo hayo ambapo ndani ya siku 21 ije na Mkakati wa Kitaifa kuhakikisha wanadhibiti changamoto hiyo.
Waziri huyo Masauni ameeleza matukio zaidi 170 ndani ya mwezi mmoja na waliokamatwa ni zaidi ya 150 kezi zao zipo kwa Ofisi ya Mkurungenzi wa mashtaka, wengine Makahakamani na ofisi ya Mpelelezi
"Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Rais Samia imeguswa na mauaji ya kikatili yanayoendelea nchini inawapa pole ndugu jamaa na Watanzania kwa kuondokewa na ndugu zao," amesema.
Ameongeza kuwa chimbuko la kikao hicho ni kutokana na maelekezo ya Rais Samia nankufanya tathimini.
Waziri huyo amefafanua kuwa vyanzo vya mauaji hayo asilimia 30 ni urithi wa mali, masuala ya mapenzi,kugombania mali, visasi, ushirikina, ulevi na kujichukulia sheria mikononi.
Ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kuhusiana na matukio hayo kwani masuala hayo sio la Jeshi la Polisi peke yake ni pamoja Wadau wengine.
Pia Waziri Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha wahusika wa mauaji ambao hawqjakamatwa katika maeneo mengine wanakamatwa mara Moja.
No comments:
Post a Comment