Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi.
Na John Mapepele
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi amesema filamu hiyo ni lango linalokwenda kufungua maendeleo kwenye kila sekta hapa nchini.
Akizungumza leo Mei 13, 2022 kwenye Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali jijini Tanga. Dkt, Abbasi ametoa wito kwa Maafisa Habari kuitangaza na amemkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali nakala ya filamu hiyo ili isambazwe nchini kupitia kwa maafisa hao.
Akitaja baadhi ya faida ya filamu hiyo amesema inakwenda kutazamwa na zaidi ya watu bilioni moja katika kipindi kifupi.
Aidha, amesema katika uzinduzi uliofanywa nchini Marekani ambako ni soko kuu la utalii wa Tanzania Rais Samia ameweza kukutana na viongozi matajiri namba moja katika sekta mbalimbali ambao wameonyesha nia ya kuwekeza hapa nchini.
Ameongeza kuwa filamu hiyo ya kihistoria, imetengenezwa katika kiwango cha kimataifa na wataalam nguli duniani ambao pia wanamitandao mikubwa ya kuisambaza.
Ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais kwa kazi kubwa aliyofanya na kuwaomba maafisa Habari na watanzania kwa ujumla kumwombea katika kazi kubwa anayoifanya ya kuitangaza na kufungua Tanzania duniani ili kuvuta wawekezaji na watalii nchini.
"Nampongeza Rais kwa kushiriki moja kwa moja katika kuitengeneza filamu hii haikuwa kazi rahisi" amesisitiza Dkt. Abbasi
Kauli mbiu ya kikao hicho ni " Mawasiliano ya Kimkakati nyenzo muhimu kufanikisha sensa ya Watu na Makazi 2022"
Kikao kazi hicho kimefungwa rasmi na Waziri wa TAMISEMI Innocent Lugha Bashungwa ambaye amesisitiza Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kusemea mafanikio ya Serikali.
No comments:
Post a Comment