KATIKA kukabiliana na majanga wakati wa ujenzi, Benki ya NMB kwa kushirikiana na baadhi ya makampuni ya bima nchini inatoa bima kwa miradi ya ujenzi dhidi ya majanga yanayoweza kuathiri utekelezaji wa miradi hiyo.
Unaweza ukabima;
•Mwanzo hadi mwisho wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi
• Sehemu ya mradi wa ujenzi
Kwa mujibu wa NMB, bima hiyo itamlinda mteja dhidi ya majanga yanayoweza kutokea kutokana na miradi ya ujenzi inayofanywa na makandarasi kama barabara, madaraja, uchimbaji madini, ufungaji na usimikaji wa mitambo.
Inashughulika pia, uharibifu wa mitambo ya uendeshaji na uzalishaji, na kukinga watu wengine wanaozunguka mazingira ya mradi wa ujenzi.
“Bima hii itamkinga na hasara itokanayo na majanga yaliyonje ya uwezo wa mteja mfano; mafuriko, dhoruba, kupoteza kipato n.k.
Vile vile, bima hii haitashughulika na majanga yatokanayo na vita, uvamizi, vita vya wenyewe kwa wenyewe au shughuli za kivita, mionzi au madhara ya nyuklia, sumu au uchafuzi unaotokana na mionzi” imesema sehemu ya taarifa kuhusu bima hiyo.
Pia, ukoseaji wa mahesebu, miundombinu mibaya/iliyokosewa, uharibifu na adhabu, uchakavu wa kawaida , uzoroteshaji na kupoteza thamani.
Janga litakapotokea, basi toa taarifa kwenye tawi la NMB lililopo karibu au kupiga simu kituo cha huduma kwa wateja namba 0800 002 002 bure!
Kwa barua pepe, tuma kwenda bancassurance@nmbbank.co.tz
No comments:
Post a Comment