Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mamlaka
ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) imezipiga faini Kampuni
nne za bima kwa kukiuka kanuni, taratibu na sheria zinazoongoza
uendeshaji wa huduma za bima.
Kampuni
zilizopigwa faini ni Insurance Group of Tanzania (IGT), Jubilee
Insurance, Kampuni ya Resolution pamoja na Kampuni ya UAP.
Akizungumza
na wanahabari jijini humo Kamishna wa Bima Nchini, Dkt. Baghayo Sagware
amesema kampuni zimepigwa faini kutokana na kukiuka taratibu na sheria
ulipaji fidia kwa wateja pale wanapopata majanga.
"
TIRA ina jukumu la kusimamia shughuli za bima, kutoa ushauri kwa
Serikali hivyo leo tunasikitika kutoa taarifa ya mwenendo usiofaa wa
kampuni nne za bima," amesema Dkt. Saqware.
Amebainisha
kuwa TIRA Oktoba Mosi mwaka jana na Februari 15 mwaka huu ilipkea
malalmiko 48 kutoka kwa wateja wa Kampuni ya IGT na kwamba walibaini
ukiukaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa shughuli za bima ikiwemo
kifungu namba 166 (1) cha sheria ya bima nchini.
Kamishna
Saqware amesema kufuatia ukiukwaji huo kampuni hiyo imepigwa faini ya
Sh Millioni 20 ambapo Mwenyekiti wa Bodi, Afisa Mtendaji Mkuu, Afisa
Fedha Mkuu pamoja na Meneja wa Madai na Fidia kila mmoja wakitakiwa Sh
Mil 5.
Amesisitiza kuwa Kampuni ya Jubilee Insurance imepigwa faini ya Sh Mil 5 ambayo imeshlipwa ikiamuru
kampuni hiyo kulipa fidia ya Euro mill 511 kama inavyodaiwa na Wizara
ya Maji baada ya kampuni ya ukandarasi ya Spencon kushindwa kutimiza
wajibu wake wa kimkataba wa miradi ya maji wenye mkataba namba
ME-011/2011-2012/W/O5 kwa Mamlaka ya Maji ya Mji wa Kigoma ambao ulikua
umepewa Kinga na kampuni ya hiyo.
Ameongeza
kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jubilee Insurance amepigwa faini
ya Sh Mil 10 kwa kutofuata sheria na taratibu za bima hivyo kuchafua
taswira ya soko la bima nchini.
Kamishna
Dkt. Saqware amefafanua kuwa Kampuni ya Resolution imepigwa faini baada
kubainika kuwa na mwenendo mbaya wa uendeshaji hivyo Afisa Mtendaji
Mkuu anatakiwa kulipa Sh Mil 5 na kwamba TIRA imeiwekea zuio la
kuendelea kufanya biashara na matangazo ya bima kuanzia leo na kuitaka
kuendelea kulipa madai yote yaliyopo na yatayokuja kuepuka kufutiwa
leseni ya biashara.
Pia amesema Kampumi ya UAP
imepigwa faini ya Sh Mil 30 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kushindwa
kushughulikia malalamiko ya wateja kwa haraka hivyo imeagizwa kulipa
fidia ndani ya siku 7.
Aidha, Mamlaka hiyo
imetoa onyo kwa kampuni za bima kuacha tabia ya kutoshughulikia wateja
wanapowasilisha malalamiko yao zitakazobainika zitachukuliwa hatua kali
za kisheria.
Wakati huo huo, TIRA imewaasa
Watanzania kuendelea kutumia huduma za bima na kuwasilisha malalamiko
yao kwa Kamishna wa Bima wanapoona hawatendewi haki na kampuni za bima.
Kwa
upande wake, Meneja Utekelezaji Sheria na Kushughulikia Malalamiko wa
TIRA, Jailo Mgavilenzi amesema kuwa Kampuni ya Jubilee ilikwenda kinyume
cha sheria za Bima kwa kumlipa fidia dalali badala ya benki waliyokuwa
wakiituma wateja kupata huduma za bima.
No comments:
Post a Comment