Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa amewataka waombaji wa nafasi za muda za ukarani na usimamizi wa Sensa katika mfumo wa maombi wa kielektroniki inayotarajiwa kufanyika hapa nchini Agosti 23 mwaka huu, kujaza fomu za maombi kwa uhakika ili kujiweka kwenye nafasi ya kupata ajira hizo za muda.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Dkt. Chuwa alisema maombi mengi yaliyotumwa yameonekana kuwa na changamoto ambazo amezitaja kuwa ni pamoja na kutojaza taarifa sahihi kama vile barua pepe na namba za simu na hivyo kushindwa kupokea neno la siri na taarifa nyingine muhimu za kumwezesha mwombaji kuendelea kukamilisha maombi yake
"Katika Maombi yote tumegundua baadhi ya changamoto ambazo waombaji wamekuwanazo ni kutokujaza taarifa sahihi kama vile barua Pepe na namba za siku na hivyo kushindwa Kupokea neno la Siri na taarifa nyingine muhimu za kumuwezesha Mwombaji kuendelea kukamilisha Maombi yake," alisema Dkt Chuwa.
Aidha akieleza changamoto nyingine waombaji Kutokuwa na baadhi ya taarifa Kama vile namba ya kitambulisho Cha Taifa Cha NIDA,Kutoambatanisha nyaraka za lazima kama vile cheti cha kuzaliwa na nyengine waombaji kuwa Katika maeneo yenye Mtandao hafifu hivyo kupelekea kupata tatizo la kutuma na kuhuisha Maombi.
Akizungumzia hali halisi ya zoezi zima Dkt Chuwa alisema kuwa hadi kufikia tarehe 9 Mei 2022 maandalizi ya Sensa yamefikia asilimia 81 huku maandalizi ya zoezi la kuwasajili makarani na wasimimizi wa Sensa yakiwa yamefikia asilimia 51.
"Tarehe 5 Mei Mwaka huu serikali ilitangaza rasmi kuanza kupokea maombi ya kazi za muda za makarani na wasimimizi wa Sensa ya Watu na makazi itakayofanyika Agosti 2022 kwa Mfumo wa Kielektroniki,"alisema Dkt Chuwa.
"Hadi Sasa Ofisi ya Takwimu NBS imeshapokea Maombi ya waombaji 119,468 ambapo waombaji 46,159 ni waajiriwa kutoka katika sekta ya umma na binafsi,"alisema.
Pia Dkt Chuwa alisema waombaji 14,393 wamejiajiri wenyewe na waombaji 58,916 ni wale ambao hawana ajira.
May 10, 2022
Home
Unlabelled
Waombaji nafasi za ukarani wa Sensa watakiwa kujaza fomu za maombi kwa uhakika
Waombaji nafasi za ukarani wa Sensa watakiwa kujaza fomu za maombi kwa uhakika
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment