HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 24, 2022

SHERIA MPYA YA HABARI ZANZIBAR YANUKIA

 


Mwanahabri nguli Zanzibar Haura Shamte.

 

Na Talib Ussi, Zanzibar

 

Baada ya safari ndefu iliyofatiwa  na makongamano ya kujadili kupatikana Sharia mpya ya Habari Visiwani Zanzibar, hatimae wanahabri wa Zanzibar wanaonekana kuwa na matumaini makubwa ya kupatikana kwa sheria hiyo hivi karibuni.

Kwa miezi kadhaa imeshuhudiwa dhamira  na juhudi njema  za kuhakikisha juhudi za kupatikana sheria mpya ya habari zinaonekana wazi wazi.

Baadhi ya taasisi kama vile internews kupitia mradi wake wa boresha habari kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) Zanzibar kimekuwa kikiwajengea waandishi wa habari uwezo katika kupigia kelele upatikanaji wa sheria mpya ya habari Zanzibar.

Haura Shamte ni miongoni mwa waandishi nguli Visiwani Zanzibar ambaye anasema kuwa anaimani kubwa kuwa safari ile ya muda mrefu ya kudai sheria mpya ya habari sasa inaelekea kuzaa matunda.

Akiwa katika moja ya mikutano ya kupitia sheria hizo ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania alisema kwa mujibu ya watendaji mbali mbali Serikali ya mapinduzi Zanzibar kuwa mswada huo umeshafika ngazi ya makatibu wakuu na inategemewa kikao cha baraza lijalo utapelekwa kama mswada wa sheria.

“Tunaimani mawazo yetu hata kama sio yote yatakuwemo kwenye mswada huo ambao ukotayari kupelekwa barazani” alisema Haura.

Kwa upande wake Mhariri wa Gazeti la Zanzibar Leo, Ramadhani Makame alimuambia mwandishi wa makala hii kuwa kutokana na viongozi wa nchi kuonyesha nia njema hanashaka upatikanaji wa sheria mpya ya habari ambayo itaaza haki ya  kujieleza na hatmae kuwa na uhuru wa habari hapa nchi.

Alisema kuwa sheria nyingi za habari hapa Zanzibar zimekuwa za zamani sana ambazo ukiziangalia zinapingana na katika ya nchi.

“Ukiangalia katika katiba na haki ya wajibu kutoa na kupokea habari lakini utazikuta sheria nyengina zinapingana na hilo, nikasema kubadilishwa kwake ni lazima” alisema Makame

Makame hakuwacha kuwausia wanataaluma wenzake na aliwaeleza waandishi kuwa  wakati waandishi wa habari wanantaka uhuru wa habari wanapaswa kuwajibika ili uo uhuru ukija uwe wa hashima.

Asha Abdi Makame akieleza matumaini yake sheria mpya ya habari alisema  sheria hiyo mpya  ambayo iko njiani kupelekwa katika chombo cha kutunga sheria  itatoa mwanya nzuri kwa waandishi kufanya kazi zao.

“Kwa  sababu sheria za habari zilizopo hapa kwetu  zinaonekana zina vizingiti ambavyo vinatukwanza katika kufanyakazi zetu lakini matumaini yangu sheria mpya zijazo zinaweza kuondoa vikwanzo katika kufanyakazi zetu” alisema Asha.

Alisema kuna baadhi ya viongozi wanajiona wao wako juu ya sheria kwa sababu wanamadaraka Fulani na kueleza kuwa anapenda sheria hiyo mpya ya habari ijayo iwe Funzo kwa viongozi kama hao ili kuwe na vipengele vya kuwadhibiti.

Alisema kazi moja ya habari ni kuibua maovu yaliomo katika jamii au nchi kwa madhumuni ya kuondolewa alidai lakini kuna baadhi ya viongozi ikiwagusa wanavamia chombo na kuanza kuwatisha waandshi.

 

“Tunataka sheria hii iwe yenye msimamo na uswa baina ya waandishi wa Serikali na wale wa binafsi kwani kazi ya ni moja, isiwe uko serikalini ukisema kitu mkuu wa mkoa au wa wilaya anakujia juu, tunataka lazima ikemee hilo”

 

 

 

Hassani Kijogoo wakili wa kujitegemea Mahakama kuu Zanzibar alisema upitishwaji wa sheria mpya ya habari utakuja kama mapendekezo yalivyotolewa na wadau yataingizwa italeta  uhuru wa habari wenye viwango vya kimataifa.

“Kama yataletwa vilele basi huo ndio uhuru wa habar” alisema Kijogoo.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo katika mchakato wa kuzipitia sheria zote zilizopitwa na wakati ambazo haziendani na  mabadiliko ya wakati uliopo sasa ambao umeingia katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.

 

Sekta ambazo zinatarajiwa kufanyiwa mapitio makubwa ya sheria zake ni ya habari na  utangazaji ambazo ni za muda mrefu na zimekuwa kikwazo kwa watendaji wa tasnia hiyo katika kutekeleza majukumu yake katika dunia ya sasa.

 

Katibu wa Tume ya kurekebishe sheria Kombo Mussa alisema serikali ipo tayari kushirikiana kwa karibu na wadau wa habari Zanzibar ili kuona sheria mpya bora ya habari inayokwenda na wakati inapatikana.

 

Alisema kazi kubwa imefanywa kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kuona sheria ya huduma za habari inapatikana ambayo itakidhi mahitaji yaliopo sasa katika kuwepo kwa uhuru wa kujieleza.

 

Kombo alizitaja sheria ya usajili wa wakala wa habari,magazeti na vitabu namba.5 ya mwaka 1988 kama ilivyorekebishwa na sheria ya namba 8 ya mwaka 1997 pamoja na sheria ya Tume ya Utangazaji ya mwaka 1997 pamoja na Marekebisho yake ya mwaka 2010 ni za muda mrefu na zinahitaji marekebisho yake.

 

Alisema sheria hizo ukiziangalia zimepitwa na wakati ambazo kwa kawaida zimepitishwa tangu mwaka 1988 kwa upande wa sheria ya magazeti licha ya kufanyiwa marekebisho mengine katika mwaka 1997.

 

“Sheria  zote mbili ile ya magazeti pamoja na Utangazaji zimetufikiya na sisi tumekubaliana kwa pamoja ni bora ziende mbele katika ngazi ya makatibu wakuu kwa kupitiwa zaidi ”alisema Kombo.

No comments:

Post a Comment

Pages