HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2022

UVCCM wazindua Kampeni ya Kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi


Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kenani Kihongosi akiongoza vijana kwenye matembezi kutoka Uwanja wa Benjamini Mkapa mpaka Viwanja vya Mwembe Yanga,katika Uzinduzi wa Kampeni ya Sensa.
 
 
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Ikiwa zimebaki siku chache kuelekea Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022 Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wamezindua rasmi Kampeni ya Uhamasishaji wa wananchi kujiandaa kikamilifu kuhesabiwa kwa kuwa na ushiriki thabiti.

Kwa kuwa sensa ni zoezi muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote duniani,Katibu Mkuu wa  (UVCCM) Taifa, Kenani Kihongosi  ameongoza maelfu ya vijana kwenye matembezi kutoka katika Uwanja wa Benjamini Mkapa mpaka kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Jijini Dar es salaam katika Uzinduzi wa Uhamasishaji wa SENSA ya Watu na Makazi ambayo itakuwa endelevu kwa nchi nzima.

katika uzinduzi huo ulishirikisha mamia ya vijana, Kihongosi amesema sensa ni msingi wa maendeleo lakini sensa inachochea maendeleo, Serikali inapokwenda kutambua watu wake ni dhahiri kwamba itapeleka kulingana na idadi ya watu wake.

Amesema sensa italisaidia Taifa katika kupanga mipango ya kuwaendeleza wananchi wake kiuchumi,kimiundombinu,kielimu,kiafya na mengineyo ambayo ni mahitaji muhimu kwa wananchi ndani ya Taifa lao.

"Tumeona baadhi ya maeneo kumekuwa na changamoto, kwanza watu walipohesabiwa mwaka 2012 ,wengine hawakuhesabiwa ,sasa Serikali inapopeleka fedha kama inalenga hospitali ,ujenzi wa shule, kuboresha huduma inapeleka kwa idadi ya namba ambayo imeandikishwa ,kumbe idadi ya watu ni kubwa ,sisi Umoja wa Vijana wajibu wetu mkubwa ni kuhakikisha tunaungana na Serikali na kuwaleza Watanzania wote wakiwemo vijana wenzetu kwamba sensa ni kitu muhimu na tunaisadia Serikali katika kusukuma ajenda ya maendeleo". Amesema Kihongosi.

Amesisitiza vijana wajitokeze kwa wingi lakini waende kuhamasisha wenzao kwasababu siku ya leo wamekuwa na vijana ambao wanatoa elimu juu ya sensa,ambapo wanawakufunzi wa sensa kutoka serikalini lakini wapo watu ambao wametunga nyimbo zinazohamasisha sensa na kueleza umuhimu wa sensa .

"Kwa hilo ni jambo la pili na jambo la tatu kampeni hii itakuwa endelevu hapa Dar es Salaam na kampeni tumezindua leo tarehe 23 mwezi wa Sita lakini tutakwenda katika mikoa yote ya Kanda ya ziwa, tutakwenda Kanda ya kaskazini , tutakwenda Kusini,lengo ni kuwakumbusha Watanzania na wajue sensa ina umuhimu mkubwa katika maendeleo lakini pia tutafika mpaka Zanzibar na kama ambavyo unafahamu Taifa letu ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeungana Tanzania Bara na Tanzania Visiwani kwa hiyo tunawajibu kufika mpaka Zanzibar kwenda kuhamasisha vijana na Watanzania kuhusiana na suala Zima la sensa.". Amesisitiza Kihongosi.

Aidha amesema katika elimu ya sensa kama kuna Wizara ambayo inahusika na masuala ya kuratibu sensa ndio maana wameleta watalaam kutoka Serikalini ambao watagusa maeneo yote yanayohitajika kuhusu sensa ,waeleza kwanini kuna sensa na inahesabiwa kwa Watanzania na kwanini pia Wananchi wahesabiwe maana Watanzania wataenda kufahamu kumbe wakihesabiwa

No comments:

Post a Comment

Pages