Akizungumza
baada ya kupokea tuzo hiyo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema tuzo hiyo itamtia
moyo na kumpa ari Rais Samia katika kuwatumikia Watanzania.
"Kitendo
cha kumpatia tuzo mnamtia moyo, mnapa ari ya kuwatumikia Watanzania,
lakini pia mnamtia ari ya kutimiza malengo yenu akinamama katika mambo
muhimu na ya msingi kama ambavyo nimeshasema.
"Wito
wangu kwenu msisite, msiishie hapa endeleeni kumuombea kwa Mwenyezi
Mungu, kila mmoja kwa imani yake Mwenyezi Mungu azidi kumpa afya njema
ili aweze kututumikia Watanzania," amesema.
Akiendelea
kuzungumza zaidi kuhusu tuzo hiyo, Shaka amesema aliyoyafanya Rais
Samia wanawake wanayajua hata ukiwaamsha usingizini wanakwambia
ameifungua Mtwara.
Awali
akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo hiyo, kwa niaba ya wanawake hao
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mtwara, Zuhura Farid,
amesema wanawake wa Mtwara kwa niaba ya wanawake wengine wote
wanampongeza Rais Samia kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya.
"Hivyo
tunaomba tukukabidhi zawadi hii kwa heshima na taadhima tunaomba
umfikishie zawadi hii mama na umwambie asichelewe kufika Mtwara aje
atuone kinamamma," amesema.
No comments:
Post a Comment