Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodrieguez Parrilla mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 29 Juni 2022 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodrieguez Parrilla amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 29 hadi 30 Juni 2022.
Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mhe. Perrilla amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula.
Wakati wa mapokezi hayo, Mhe. Balozi mulamula ameeleza madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha na kukuza ushirikiano wa kihistoria ulioasisiwa na Wasisi wa mataifa hayo mawili, Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Fidel Castor aliyekuwa Rais wa kwanza wa Taifa la Cuba.
Tanzania na Cuba zimeendelea kushirikiana katika maeneo ya afya, elimu, viwanda, na biashara. Pamoja na maeneo hayo serikali hizo mbili zinatarajia kufungua maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za Kilimo, utalii, ushirikiano katika usimamizi wa masuala ya zimamoto na uokoaji, utamaduni na michezo.
Aidha, akiwa nchini Mhe. Parrilla pamoja na mambo mengine atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
No comments:
Post a Comment