Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) akimkabidhi injini ya boti Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (kushoto) aliyeipokea kwa niaba ya wananchi wa Pangani wakati wa hafla ya kukabidhi injini hizo iliyofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara zilizopo kwenye jengo la Benki ya NBC Jijini Dodoma.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema kuwa inatarajia kununua Boti zaidi ya 300 kutokana na kiasi cha fedha cha shilingi bilioni 21 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan zitakazotumiwa na wa vuvi wa Kanda ya Pwani.
Hayo yamesemwa Juni 24,2022 Jijini hapa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki katika hafla fupi ya kukabidhi mashine au injini tatu za Boti zenye thamani ya shilingi milioni 33 kwa Wabunge wa majimbo ya Pangani, Mtwara Mjini na Iringa Vijijini kwa niaba ya wavuvi katika maeneo yao.
Amesema lengo la Injini hizo ni kuwawezesha wavuvi waweze kuingia katika maji mengi na kuweza kufuata rasilimali hasa samaki ambazy zitasaidia kutatua changamoto wa vuvi hao baharini kutokana na ule utaratibu mita mita 50 wa kuvua samaki.
Waziri Ndaki amefafanua kuwa wanatarajia kununua boti 25 kwa kipindi cha kwanza ambapo kipindi cha pili wataongeza 70 na kufikiwa idadi ya boti hizo 300 ambazo zitawarahisishia wavuvi kutimiza majukumu yao na kuongeza kipato chao na Taifa.
" Tuna mshukuru Rais Samia kwa kutupatia fedha hizi. Tunaamini kwa matumizi mazuri ya fedha hizi tutaongeza uzalishaji wa samaki na kuongea kipato kwa wananchi nao wakiongeza kipato Taifa litaongeza kipato chake, tutakuwa na uwezo wa kuuza kwenye viwanda vyetu," amesema Waziri Ndaki.
Ameongeza kuwa wanachangamoto nyingi kwenye masuala ya Uvuvi kando kando ya bahari, maziwa na maeneo mengine wanayo vua samaki lakini wanajatibu kuzitatua moja baada ya nyingine.
Awali Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dk. Nazael Madala
amesema kuwa kwenye uchumi wa bluu jukumu lao Uvuvi na hiyo ni sehemu ya kuwaongezea mwenendo wavuvi ili waweze kunufaika na uchumi huo wa bluu.
Kwa upande wake Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Pangani ameishukuru wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano huo huku akisema vifaa hivyo vitawasaidia wananchi wake wavuvi.
"Naishukuru wizara kwa kuamua kujenga soko la samaki Pangani na kwamba wanapangani wataendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara," amesema.
Naye mbunge wa Mtwara Mjini, Hassan Mtenga kuwa ameiomba Wizara hiyo kuendelea kuwawezesha wavuvi vifaa vingine vya uvuvi kama vile majokofu ya kuhifadhia mazao ya uvuvi ili wanapofanya shughuli zao za kusafirika wahidhi sehemu salama.
No comments:
Post a Comment