HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 12, 2022

WACHEZAJI WA MPIRA WA KIKAPU KUTOKA MAREKANI WAENDESHA MAFUNZO KWA VIJANA NA WATOTO

 Tarehe 12 Julai, Ubalozi wa Marekani kwa kushirikiana na Taasisi ya Familia ya Brogdon, Jr. NBA Africa na Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park wamewakaribisha wachezaji wa mpira wa kikapu wa Kimarekani Myles Turner, Tim Frazier na Antony Tolliver. Wachezaji hao wameendesha kambi ya mafunzo ya mpira wa kikapu kwa vijana na watoto 200 pamoja na makocha, katika kituo cha Michezo cha Jakaya Mrisho kama sehemu ya Programu ya Diplomasia kupitia Michezo, inayolenga kujenga mahusiano ya kimataifa kupitia mabadilishano ya kimichezo.







No comments:

Post a Comment

Pages