Mwenyekiti
wa chama Cha ACT Wazalendo Mhe. Juma Duni Haji amesema moja
katika masuala yanayoleta matatizo makubwa katika visiwa vya Unguja ni
umiliki wa ardhi na makaazi.
Hayo
aliyasema mbele ya timu ya uhamasishaji wa zoezi la Sensa pamoja na
wajumbe wa mkutano mkuu wa ACT Wazalendo wa mkoa wa kaskazini A
Unguja katik kijiji cha Shangani.
Duni
alisema umiliki wa ardhi na ongezeko la watu visiwani ni jambo ambalo
linahitaji kuangaliwa kwa makingi na kulipatia ufumbuzi wakudumu.
Hata hivyo alisema zoezi la sensa yawatu na makaazi linaweza kuleta ufumbuzi wa kudumu.
Aidha alitaka wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa ili kurahisisha mipango ya maendeleo ambayo itamnufaisha kila mwananchi.
Mapema
katika kikao hicho kaimu Naibu katibu mkuu wa ACT Wazalendo Salim
Abdalla Bimani ameiomba tume hiyo kushirikisha vijana wa vyama vyote
katika kazi ya i kuhesabu watu badala kuwemo watendaji wa chama
kimoja..
Alisema miaka
kumi iliyopita hapakuwa na mashirikino ya masuala ya sensa kwani
yalionekana kama ni zoezi la siasa ya upande mmoja.
Alisema Mara hii kunaonekana kutakuwa na mashirikiano makubwa ya kufanikisha zoezi hilo.
Hivyo
alisema ni vyema zoezi hilo kushirikisha vyama vyote vya siasa badala
ya hivi sasa kuonekana kuwepo sura ya watendaji wa upande mmoja
"ACT
tunahitaji kushirikishwa mana bado wanaoshughulikia sensa kuna sura ya
chama kimoja ili tufanikiwe kwenye Sensa hii tunahitaji tushirikishwe"
alisema Bimani.
Aidha alisema vijana wao ndio wanaotambua watu katika shehia zao kushirishwa kwao kutasaidia kurahisisha zoezi hilo.
Kwa
upande wake afisa mahusiano ofisi ya mtakwimu mkuu bi Safia Abdalla Ali
alisema serikali imekabiliwa na shughuli kubwa kuhesabu watu yenye
lengoo la kupata takwim sahihi zitazoiwezesha serikali na wadau wengine
kupanga mipango kwa usahihi.
Alisema
zoezi hilo litakuwa ni la nchi nzima kwa sasa wapo katika zoezi la
uhamasishaji na kuelimisha umma juu ya umuhimu wa sensa.
Pia
alisema sensa ya watu na makaazi ni moja zoezi muhimu linalokusanya
taarifa za kila mtu aliyelala ndani ya mipaka ya nchi usiku wa kuamkia
siku ya sensa.
No comments:
Post a Comment