NA TATU MOHAMED
CHUO
Kikuu cha Mzumbe kimekuja na ubunifu wa mkojo wa Sungura kutumika kwa
kilimo cha matunda na mbogamboga ili kufukuza wadudu waharibifu.
Katika
kufanya tafiti zake, imegundulika kuwa mkojo wa Sungura unaharufu kali
hivyo sio rafiki kwa wadudu hasa wale waharibifu katika mboga zenye
jamii ya maua na matunda.
Akizungumza
katika maonesho ya 46 ya biashara ya Kimataifa (DITF) maarufu kama
'Sabasaba' yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Mwanafunzi wa Sayansi ya
Uzamili Chuo Kikuu cha Mzumbe, Nelson Kissanga alisema wamekuja na
ubunifu huo ambao utawasaidia wakulima kutokupata hasara kwa mazao yao
kuliwa na wadudu.
"Wadudu
ni waharibifu katika mbogamboga na mboga zenye jamii ya maua pamoja na
matunda kwani wanapenda kuvutiwa sana na mvuto wake katika kufata
harufu nzuri ya maua hasa yanapochanua.
"Kwahiyo
mkojo wa Sungura ni mbadala wa utumiaji wa kupuliza madawa katika
mbogamboga na matunda ambapo yanakuwa na madhara kwa watu wengi. Pia ni
fursa kwa watu wengi kwani unapowafuga Sungura na kupata mkojo
wao,mfugaji anapaswa kujenga banda la juu (ghorofa)kidogo hivyo
wanapokojoa kunakuwa na kinga zinazokuwa zinakinga mkojo wao," alisema
Kissanga.
Aidha alisema
mkojo huo hauna shida yoyote kwa watumiaji kwani hauna kemikali yoyote,
unakuwa ni mkojo halisi unaotoka kwa Sungura.
Aliongeza
kuwa, hiyo itawasaidia watu kubadilika kutumia vyakula venue kemikali
na kula vitu vya asili kwani gharama za kemikali katika kununua
zinakuwa juu kuliko mkojo wa Sungura.
"Tumeongeza
mnyororo wa thamani wa mfumo huu wa mkojo wa sungura ni rafiki wa
mazingira na rahisi kutumia tunaomba watu wawe tayari kuupokea na
kuutumia waone kama fursa," alisisitiza.
Kwa
upande wake, Mwanafunzi wa Chuo cha Mzumbe Maziku Maziku, alisema
wamebuni teknolojia ya Unikopa katika kusaidia wanafunzi kukopa mkopo
wa simu,fedha na laptop.
Alisema
unikopa katika vyuo vikuu imekuja baaada ya mikopo kuonekana wanafunzi
wanakuwa na changamoto mbalimbali katika kupata mitaji.
"Wanafunzi
wengi wanakutana na changamoto ya kupata fedha kwa urahisi zaidi kwani
wanakopeshwa hawana dhamana ya nyumba na fedha kwahiyo mfumo huu ni
rahisi kwao kwani hauna riba yoyote,"alisema
Alisema
mpaka sasa wanawanafunzi 1320 ambao wamejisajili katika mfumo huo
kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDOM), Mzumbe, Ardhi pamoja na
UDOM.
No comments:
Post a Comment