Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya CRDB, Moureen Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 14, 2022 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Elimu ya Bima ya Vyombo vya Moto iliyopewa jina la “Kuwa Shua”, uliofanyika katika Gereji ya MacAuto Sinza.
Mkuu
wa Kitengo cha Bima wa Benki ya CRDB, Moureen Majaliwa akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 14, 2022 wakati wa
uzinduzi wa Kampeni ya
Elimu ya Bima ya Vyombo vya Moto iliyopewa jina la “Kuwa Shua”,
uliofanyika katika Gereji ya MacAuto Sinza. Kushoto ni Meneja Uendeshaji
Huduma za
Bima Benki ya CRDB, Tumaini Frank na Meneja Mauzo Oreyx Tanzania, Fredy
Mcharo.
Na Mwandishi Wetu
Benki
ya CRDB leo imezindua kampeni maalum ya elimu ya bima ya vyombo vya
moto iliyopewa jina la ‘Kuwa Shua’ katika hafla ulifanyika katika
gereji ya MacAuto iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya CRDB, Moureen
Majaliwa amesema lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha wamiliki wa vyombo
vya moto kukatia vyombo vyao bima ili kujikinga dhidi ya majanga.
Majaliwa
alisema pamoja na kuwa bima ya vyombo vya moto ni moja ya bima
zinazotumika kwa kiasi kikubwa bado wamiliki wengi wa vyombo vya moto
nchini hawana elimu ya kutosha kuhusu bima, jambo linalopelekea wengi
kupuuzia.
“Katika
kipindi cha kampeni maafisa wetu wa Benki watakuwa wakitembelea wateja
kuwapa elimu ya bima za vyombo vya moto, lakini pia tutakuwa tukitoa
zawadi kwa wateja watakaokata bima kupitia Benki ya CRDB,” alisema
Majaliwa.
Akielezea
kuhusu zawadi kwa wateja Majaliwa alisema wamiliki wa vyombo vya moto
watakaolipia bima kubwa ya ‘comprehensive’ watarudishiwa asilimia 5 ya
kiasi cha bima (kabla ya VAT) kama mafuta kupitia vituo vya Oryx nchi
nzima.
“Baada
ya kulipia bima, aidha kupitia tawi la Benki, CRDB Wakala, au
SimBanking, mbali ya mteja kupokea ujumbe wa sera yake ya bima, vilevile
atapokea ujumbe wenye nambari ya zawadi ambayo ataitumia kujaza mafuta
katika vituo vya Oryx,” aliongezea.
Taratibu
za usalama zinaonyesha ni sharti la lazima kwa vyombo vya moto kuwa na
bima kabla ya kuruhusiwa kuingia barabarani. Majaliwa anasema jamii
inapaswa kuchukulia kwa umuhimu huduma hiya ya bima kujikinga na majanga
ya ajali za barabarani.
Majaliwa
alisema kampeni hiyo pia inalenga katika kusaidia malengo ya Serikali
kupitia Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha ya kuongeza ujumuishi wa
Watanzania katika huduma za bima kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.
Katika
kuhakikisha kuwa kampeni hiyo inakuwa na mafanikio, Benki ya CRDB
imeandaa Tamasha la Elimu ya Bima ya Vyombo vya Moto litakalofanyika
Viwanja vya Posta, Kijitonyama, siku ya Jumamosi tarehe 17 Septemba
2022.
Tamasha
hilo linakusudia kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wa vyombo vya moto;
kampuni za bima, gereji, maduka ya vifaa, na Mamlaka ya Usimamizi wa
Bima (TIRA), Msuluhishi wa Migogoro ya Bima, na Jeshi la Polisi.
Meneja
Uendeshaji Huduma za Bima Benki ya CRDB, Tumaini Frank aliwakaribisha
wamiliki wa vyombo vya moto kushiriki katika tamasha hilo ili kupata
elimu, lakini pia kukutana na watoa huduma mbalimbali.
No comments:
Post a Comment