MTAFITI na mtaalam wa tiba asili, Dk. Khalid Hussein Bwenya, akimkabidhi dawa asili Juma Selemani ambaye ni muathirika wa dawa za kulevya.
Dk. Khalid Hussein Bwenya.
Na Mwandishi Wetu
MTAFITI na mtaalam wa tiba asili, Dk Khalid Hussein Bwenya amegundua dawa asili iliyokuja kuchukua nafasi ya dawa nyingine za kisasa ambazo malengo yake ni kuiondoa jamii katika madhara hao ya matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinarudisha nyuma maendeleo badala ya kusaidia nguvu kazi ya Taifa.
Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari, Kigamboni jijini Dar es Salaam Dk Khalid Bwenya aliweka bayana malengo yake mgunduzi na mtafiti huyo ni kuisaidia serikali kupunguza gharama kubwa za kukabili tatizo la mateja.
Alisema mateja ni janga kwa taifa na Dunia kutokana na kutokuwa na mchango kwa ujenzi wa Taifa, zaidi ya hayo ni mzigo na kero kwa familia na jamii kutokana na tabia zao za uhalifu na vitendo vya uvunjifu wa sheria kama wizi, ukabaji na uharibifu wa mali.
Kwa kuliona na kulitambua tatizo hilo, Dk Bwenya amekuja na jawabu la kukabili uteja kupitia dawa ya asili ambayo ndani ya siku 15, mraibu anarejea katika hali yake kama ilivyokuwa kabla ya kutumia mihadarati.
Dk Bwenya mtaalam na mtafiti wa tiba za asili anasema dawa hiyo ni suluhisho la tatizo la uteja, ugunduzi uliopata suluhu yake tangu mwaka jana.
Alisema dawa hiyo inatokana na mchanganyiko wa matunda mbalimbali na mitishamba ipo katika mfumo wa kimiminika ambako mbali na kutibu tatizo la uteja pia linatoa sumu mwilini, inaondosha gesi tumboni, kutoa sumu kwenye ubongo na mengineyo mengi.
Kuhusu ufanisi wa dawa hiyo.
Dk. Bwenya alisema dawa hiyo aliyoifanyia utafiti kwa zaidi ya miaka 20 ina uwezo mkubwa wa kukabili tatizo la uteja kwa siku 15.
Anasema muda huo wa siku 15 unatosha kuleta matokeo chanya iwapo muathirika atatumia dawa hiyo kama alivyoelekezwa.
"Kama muathirika wa dawa za kulevya (Haijalishi ametumia dawa za kulevya kwa miaka mingapi) atazingatia maelekezo ya utumiaji wa ndani ya siku 15, matokeo yataanza kuonekana," alisema Dk. Bwenya.
Alisema uchunguzi wao umebaini kwamba dawa hiyo ya ikitumika ipasavyo ina matokeo mazuri na kwa haraka ukilinganisha na dawa za kisasa.
Kuhusu athari za utumiaji wa dawa zake, Dk Bwenya alisema haina usumbufu wa aina yoyote kwa mtumiaji.
Alisema tofauti na dawa za kisasa ambazo husababisha mning'inio (hangover) kwa mtumiaji kwa upande wa dawa zake haisababishi hali hiyo.
Aidha ili kufanikisha matarajio yake ya kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya, anajipanga kuwa na shamba la ekari 500 kwa ajili ya kupanda miti ya aina mbalimbali ambayo ni tiba ya maradhi mengi ambako pia ataweka kiwanda kikubwa kwa ajili ya uzalishaji wa dawa.
Alisema utafiti wake ameufanya kwa kusoma vitabu mbalimbali, majarida sambamba na kuongea wataalam wengi na kufanikiwa kutengeneza dawa hiyo ambayo ni mkombozi kwa vijana wa kitanzania.
Dk. Bwenya alisema utafiti wake wa kwanza alianzia Afrika Kusini mwaka 2001 katika jiji la Cape town ambako amejifunza mambo mengi ambayo yalifungua njia ya kufikia suluhisho la upatikanaji wa dawa ambayo ni mkombozi kwa vijana na jamii kwa ujumla.
"Kwa sababu kazi nnayofanya ni kwa ajili ya jamii ya watanzania na waafrika wote, naiomba serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi waniunge mkono kwani jambo ninalofanya linatuhusu sote, nawaomba wanishike mkono katika hili," alisema Bwenya.
Naye mzazi wa Juma Selemani, Selemani Saleh ambaye ni muathirika wa dawa za kulevya alisema mtoto wake huyo alikuwa tegemezi lake ambako alitumia dawa za hospitali kwa zaidi ya miaka sita lakini hakupata nafuu ila hivi karibuni alipokutana na Dk. Khalid akampatia dawa na hivi sasa mtoto wake anaanza kupata nafuu.
Saleh alisema mtoto wake huyo kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya aliwahi pia kufanyiwa operesheni ya utumbo.
Nilikutana na Dk Khalid Kigamboni akitafuta nyumba kwa ajili ya kupanga ili aweke kituo chake, ndipo alipopata nafasi ya kukutana naye.
Naye Juma Selemani alisema baada ya kutumia dawa ya Dk Khalid kwa siku ya kwanza aliharisha na kutapika lakini baadaye alianza kupata hamu ya kula, akaanza kupiga chafya na mwili kuanza kupata nguvu.
Aliwaasa vijana wenzake kuachana na matumizi ya dawa za kulevya kwani wao ni nguvu kazi inayotegemewa na Taifa.
Selemani alisema kwa vijana wenzake waliochoka kuvuta unga na kujutia nafsi zao, wajitokeze kupata dawa bila gharama yoyote.
No comments:
Post a Comment