HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2022

Ocode yawajengea darasa la kisasa wanafunzi wa shule ya msingi kiluvya

 

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James, akikata utepe kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa chumba cha darasa la awali katika shule ya msingi Kiluvya kushoto kwake ni mkurugenzi wa Shirika la Ocode Joseph Jakson.


Na Victor Masangu, Kiluvya 

Shirika lisilokuwa na kiserikali la Organization for Community Development (OCODE) katika kuunga mkono juhudi zinazofanya na serikali katika kuboresha sekta ya elimu imejenga darasa la awali kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaosoma katika shule ya msingi Kiluvya.

Hayo yamebainisha na Mkurugenzi wa Shirika hilo la OcodeJoseph Jakson  wakati wa halfa fupi na kukabidhi rasmi darasa hilo jipya ambalo limejengwa kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wa awali ambao wanasoma katika shule hiyo kupata fursa ya kujifunza kusoma kuhesabu na kuandika.

Katika sherehe hizo za makabidhiano zimeweza kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na walimu kutoka shule mbali mbali wakiwemo walezi pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.

"Katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu tumefanikiwa kujenga vyumba vinne vya madarasa kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa awali katika manispaa ya ubungo,alisema Mkurugenzi huyo.


Aidha alisema kuwa shirika lao  kwa kipindi cha miaka minne wameweza kujenga madarasa katika shule za msingi.Goba,Kiluvya,Malamba mawili pamoja na Kibwegere na yamegharimu kiasi cha zaidi ya milioni 113.

Katika hatua nyingine alisema lengo lao kubwa ni kuwasaidia wanafunzi kwa kuwajengea miundombinu mizuri ya madarasa kwa ajili ya kuwasaidi kupata elimu ambayo ni Bora.

"Mbali na kukabidhi chumba hiki cha darasa la awali pia tumeweza kukabidhi madawati,viti pamoja na meza kwa ajili ya walimu waweze kufundisha katika mazingira mazuri,"alisema Jakson.

 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo alilipongeza shirika Hilo la Ocode kwa kujikita na kusaidia kuboresha zaidi sekta ya elimu  hasa kwa wanafunzi wa awali.

Alisema serikali kuwa serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu hivyo juhudi ambazo zinafanywa na Ocode zinapelekea kuleta matokeo chanya ya kuwasaidia watoto wadogo kupata elimu bora kuanzia ngazi za chini.

Katika hatua nyingine aliwataka wazazi na walezi kuwalinda na kuwatunza watoto wao ili kuachana na vitendo vya wizi na uhalifu na badala yake wahakikishe wanawapatie elimu iliyo Bora.

"Wazazi na walezi mnapaswa kuhakikisha mnawalinda na kuwatunza watoto wenu ili waachane kabisa na vitendo vya uharifu na wizi sio anaiba vitu anakuletea na wewe unafurahia tu hii tabia sitaki kuisikia kabisa kikubwa ni watoto wetu kupata elimu,"

"Rais wetu wa awamu ya sita amekuwa mstari wa mbele katika kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu hivyo katika kuunga juhudi hizi Ocode wameweza kujenga madarasa ya awali  kwa ajili ya kuwasaidi watoto,"alisema Kheri .

Naye mkuu wa shule ya msingi Kiluvya Leah Sanga alisema mafunzo ambayo wamepatiwa na Ocode pamoja na ujenzi wa madarasa kumeweza kuwa mkombozi katika kuwasaidia watoto hao waweze kusoma na kuandika.


No comments:

Post a Comment

Pages