HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 02, 2022

TSB yakagua singa za mkonge zinazosafirishwa nje


Ofisa Udhibiti Ubora wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Emmanuel Lutego akikagua ubora wa singa za mkonge katika Bandari ya Tanga kabla ya kusafirishwa nje ya nchi, kulia ni Ofisa Habari Msaidizi, Lucy James. (Picha na mpigapicha wetu).

 

Na Mwandishi Wetu, Tanga

BODI ya Mkonge Tanzania (TSB) imefanya ukaguzi wa singa za mkonge (fibre) zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi zinazopita katika Bandari ya Tanga.

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Afisa Udhibiti Ubora wa TSB, Emmanuel Lutego amesema ukaguzi huo ni wa kawaida ambao hufanywa mara kwa mara na maafisa udhibiti ubora baada ya singa hizo kupelekwa bandarini na wakulima, wafanyabiashara au wazalishaji kupitia kampuni zao mbalimbali.

Amesema ubora wa singa hupangwa kwa madaraja ambapo madaraja hayo ni Daraja Na. 1, A, 2, 3L, 3S, UG, SSUG, Tow I na Tow II na mengineyo ambapo singa zinazokidhi vigezo hivyo huruhusiwa kusafirishwa na ambazo hazijakidhi huzuiliwa.

“Baada ya ukaguzi na kuridhika na ubora wa daraja husika Bodi ya Mkonge hutoa cheti cha ukaguzi kupitia Mfumo Jumuishi wa Taarifa ya Usimamizi wa Biashara za Kilimo (ATMIS).


“Singa hizi husafirishwa nchi mbalimbali ikiwamo Senegal, Nigeria, Spain, Saudiarabia, China, India, Misri, Ivory Coast, Libya, Togo, Benin, Pakistan, Morocco na Ufilipino ambapo,” amesema Lutego.

Aidha, amesema singa hizo huenda kutengeneza bidhaa kulingana na nchi inayokwenda ikiwamo ujenzi wa nyumba, utengenezaji wa magari, mazuria, kamba za lifti, kamba za kawaida, vikapu na mapambo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages