Na John Richard Marwa
Wakati Simba wakishuka leo dimbani kumenyana na Ruvu Shooting mtanange wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara katika Dimba la Benjamin Mkapa, mzuka umepanda kwa urejeo wa kiungo fundi Clatous Chota Chama.
Simba ilimkosa Chama katika michezo mitatu Iliyopita ambapo alikuwa akitumikia adhabu kutoka Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kosa la kukwepa kusalimiana na Wachezaji wa Yanga katika mchezo uliozikutanisha klabu hizo Oktoba 23 Mwaka huu.
Akizungumza kuelekea mchezo wa leo Kocha Mkuu wa klabu ya Simba Juma Mguda amesema Chama ameshamaliza adhabu yake na yuko tayari kushuka dimbani leo.
"Kuhusu Chama ameshamaliza adhabu yake na tayari amejiunga na wenzake na Mungu akipenda leo atakuwa sehemu ya mchezo."
"Tunaiheshimu Ruvu, ni timu nzuri na ina kocha mwenye uzoefu lakini tumefanya maandalizi na tupo tayari kwa mchezo lengo likiwa ni kutafuta pointi tatu." amesema Mgunda.
Kwa upande wa Wachezaji mlinda mlango namba tatu wa wekundu wa msimbazi Ally Salim amesema kama wachezaji wako tayari kutekeleza maagizo ya benchi la ufundi.
“Sisi wachezaji tupo tayari, maandalizi yamekamilika na maelekezo tuliyopewa na benchi letu la ufundi tutahakikisha tunayafuata ili kupata pointi tatu muhimu."
"Tumeandaliwa vizuri na tumepokea kile tunachoelekezwa kutokana na mchezo ambao tunaenda kucheza. Tuko tayari kuwakabili Ruvu Shooting hapo kesho." Ally Salim
Simba wanashuka kwenye mchezo huo wakiwa na pointi 24 katika michezo 11 waliyoshuka dimbani, mabao 20 ya kufunga na matano ya kufungwa nafasi ya tatu nyuma ya vinara Yanga SC na Azam FC.
No comments:
Post a Comment