Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Meja Jenerali, Joseph Furaha
Kapwani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe za miaka 32 ya tangu kuanzishwa
kwa kamandi hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Usalama na Utambuzi, Meja Erick
Cleiphas. (Picha na Francis Dande)
Waandishi wsa habari wakimzikiliza Mkuu wa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga, Meja Jenerali, Joseph Furaha Kapwani.
Na Ramadhani Tembo
KAMANDI ya
Jeshi la Anga nchi imejipanga kuonyesha zana zake za kivita na majukumu yake
katika maadhimisho ya miaka 32 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1982, yanayotarajiwa
kufanyika jijini Mwanza Julai 23-28 mwaka huu.
Maadhimisho
hayo yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wanchi,majeshi ya ulinzi na usalama,
wananchi wa kanda ya ziwa ,mikoa ya jirani na Taifa kwa ujumla na kupata fursa
ya kuona zana mbalimbali za anga zinazotumika na Jeshi hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga, Meja Jenerali, Joseph Kapwani amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kusherehekea miaka 32
na kujitathmini kiutendaji.
“Tunatarajia
kufanya maadhimisho hayo ili wananchi wajue kazi mbalimbali zinazofanywa na
jeshi hilo na kuwahamasisha vijana wanaopenda kujiunga na Jeshi la
Anga”alisema.
Alisema
Kamandi hiyo ni moja kati ya Kamandi tatu zinazounda Jeshi la Ulinzi na Usalama
(JWTZ) ambayo inahusika na jukumu la kuhakikisha anga linakuwa salama wakati
wote kwa kutumia ndege za kivita,ndege za usafirishaji,makombora,na mizinga ya
kudungulia ndege.
Aliongeza
kuwa mpaka sasa Jeshi hilo linamafanikio makubwa na linawahakikishia watanzania
hali ya usalama wa anga itakuwa salama wakati wote.
No comments:
Post a Comment