HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 11, 2025

Tunaenda kujitegemea umeme Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua Sera ya Nishati Zanzibar 2025 na Mpango Mkuu wa Umeme 2025/2050 akisema kuwa lengo la mpango ni kujitegemea kwa nishati ya umeme ifikapo 2050.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Zanzibar leo 11 Septemba 2025, Rais Dkt. Mwinyi alisema kuwa sera hiyo na mpango mkuu umelenga ushirikishaji wa sekta binafsi katika kuzalisha umeme jumuishi kwa kutumia vyanzo mbadala badala ya kuwa kama ilivyo sasa ambapo unategemewa wa gridi ya Taifa kutoka Tanzania Bara.

Alisema umeme huo wa nyaya kupita baharini (Marine Cable), zina ukomo wa kiwango cha usafirishaji huku wa vyanzo vingine kukishindikana kuunganishwa na gridi ya Taifa hivyo kusababisha kukatika mara kwa mara na gharama kuwa kubwa hivyo kuzorota shughuli za kijamii na kiuchumi. 

“Natarajia utekekeleza wa sera ya nishati na mpango wa umeme utaongoza upatikanaji wa nishati mjini na vijiji na utendeleza miundombinu, mitambo, usambazaji na usafirishaji na mfumo wa usimamizi na udhibiti” alisema.

Alibainisha kuwa mpango utaweka mkakati wa kijamii kuhusu nishati safi na kukaribisha uwekezaji na mazingira bora ya biashara, kuchochea ukuaji wa uchumi na kulinda mazingira na mpango mkuu wa umeme 2025-2050 ni hatua muhimu kwa maendeleo ya Zanzibar.

Alisema Zanzibar haiwezi kufanikisha ndoto ya dira ya maendeleo ya Taifa  2050 bila umeme wa uhakika na kiwango cha matumizi na mahitaji ya umeme kimezidi kuongezeka Zanzibar na katika nchi yoyote maendeleo hupimwa kwa kiwango cha matumizi ya nishati hiyo.

“Tunatumia umeme kutoka Tanzania Bara na waya ulikuwa unatupatia megawati 100, baada ya miaka 33 ukaongezwa mwingine wa megawati 40 na wa zamani ukawa hautumiki hivi sasa tunatumia megawati 160 hivyo ni maendeleo makubwa ambayo lazima tuende nayo sambamba kwa kuongeza uzalishaji wa umeme, usafirishaji na ujenzi wa miundombinu.

Dkt. Mwinyi alikemea wizi wa transfoma na alibainisha kuwa si rahisi kwa mtu wa kawaida kufanya uhalifu wa namna hiyo hivyo hao  ni watu ambao wanaujua umeme na alitanabaisha kuwa kubomoa ni kazi rahisi kuliko kujenga hivyo hatua kali zichukuliwe ili wasiendelee kurudisha nyuma maendeleo.

Awali akikzungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Shaib Hassan Kaduara alilaani wimbi la wizi wa transfoma nane ndani ya miezi miwili na ameahidi kuwa watawashughulikia na wasilaumiwe kwa kitachowatokea kwani ni hujuma na hajui wafanyao hivyo hajui wana lengo gani.


 

No comments:

Post a Comment

Pages