HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 11, 2025

Ratiba mikutano kampeni ya Dkt. Mwinyi Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni mgombea wa nafasi hiyo tena katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika 28 Oktoba 2025, kutoa mwelekeo wa kampeni zake wakati atakapozungumza na wanahabari 12 Septemba 2025, Zanzibar.

Akizungumza na wanahabari, Kisiwandui Unguja, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema mgombea, Rais Dkt. Mwinyi ataeleza jinsi gani atafanya kampeni zake na nini mwelekeo wake kwa waZanzibari 2025/2030.

Mwenezi Mbeto alibainisha kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kutoa ratiba ya mikutano ya kampeni kwa wagombea hivyo 13 Septemba 2025, Dkt. Mwinyi atazindua rasmi kampeni za kuinadi Ilani mpya ya CCM 2025/2030 katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Unguja.

Mbeto alisema baada ya uzinduzi huo, 15 Septemba 2025, atakuwa viwanja vya Pujini vilivyopo  Mkoa wa Kusini, Pemba na kwa muhtasari atakuwa na mikutano 11 kila wilaya na minne ambayo itakuwa na mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Pia atakuwa anasimama na kuzungumza na makundi mbalimbali, mara ya kwanza wakati anaingia alipita kwa wavuvi wajasiramali, wafanyabiashara wadogo walihitaji masoko, mitaji na maeneo mazuri ya kufanyabiasha na hayo ameyatekeleza” alisema.

Alisema zaidi ya Tsh.Bilioni 16 zimetumika kujenga masoko kila wilaya ukiacha masoko makubwa ya kimkakati ya Kwerwekwe, Chuini, Jumbi, Macho manne na Wete na anapita katika makundi hayo na pia atakutana na wanafunzi wa elimu ya juu ambako aliahidi wote watakadahiliwa kuanza chuo wangepata mikopo wote bila kubagua.


 

No comments:

Post a Comment

Pages