HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 09, 2022

CLUB AFRICAIN YAWAONYA MASHABIKI WAKE


 

Na Mwandishi Wetu


Kuelekea mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC, Uongozi wa klabu ya Club Africain umetoa tafadhali kwa mashabiki wake.


"Bodi ya Wakurugenzi ya Club Africain inawataka mashabiki wake kuwa waangalifu, kujizuia na kutojihusisha kabisa na fujo (kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Yanga)" imeeleza taarifa hiyo.

Kupitia mtandao wa kijamii muda huu klabu hiyo imetoa tamko hilo ikiwataka wasifanye kitendo chochote cha uvunjifu wa taratibu kama waliofanyiwa wao Dar es Salaam.

Bodi hiyo imesisitiza umuhimu wa nidhamu katika kuheshimu sheria za mashindano ili kuepusha timu yao kupata adhabu kutoka (CAF).

Ikumbukwe tayari klabu hiyo imeonywa na iko chini ya uangalizi wa (CAF).

No comments:

Post a Comment

Pages