HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 09, 2022

WATAJUA SISI NI SIMBA


 

Na Mwandishi Wetu

Ni siku ya pekee na adhimu kwa Soka la Wanawake ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA kushuhudia Simba Queens wakimenyana na Mamelod Sundowns hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Soka la Wanawake Afrika CAF WCL.

Simba Queens leo wanashuka dimbani kusaka tiketi ya Fainal ya michuano hiyo mikubwa dhidi ya Mabingwa watetezi Masandawane.

Akizungumza kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa Simba Queens Charles Lukula amesema  wanawaheshimu Mamelod lakini Mamelod wanapaswa kutambua kuwa wao ni Simba.

"Tunawaheshimu Mamelod na tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini wanapaswa kutambua kuwa sisi ni Simba, hatujaja kushindana ila kushinda"amesema Lukula.

Kwa upande wa wachezaji wa Simba Queens kupitia kwa Fatuma Issah 'Densa' amesema wanaenda kuushangaza Ulimwengu.

"Wachezaji wote tuko na morali ya hali ya juu, tunafahamu ukubwa na ubora wa wapinzani wetu ila kila mmoja yuko tayari kuipamania Simba " amesema Densa.

Mchezo huo utapigwa mjini Rabat nchini Morocco majira ya saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Kila la heri Simba Queens

No comments:

Post a Comment

Pages