Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
WAZIRI
wa Nishati January Makamba amesema lengo la Mjadala kuhusu Sera,
Sheria, Kanuni na Mifumo ya Udhibiti ya Kuwezesha Nishati Safi ya
Kupikia ni kupata njia ya kufanikisha matumizi ya Nishati Safi ya
Kupikia nchini.
Makamba
amebainisha hayo leo jijini Dar es Salaam katika Mjadala wa Kitaifa wa
Nishati Safi ya Kupikia kwenye mada iliyokuwa ikihusu Sera, Sheria,
Kanuni na Mifumo ya Udhibiti ya kuwezesha nishati hiyo.
“Hili
jambo hatuwezi kwenda kulifikia bila kuwa na Sera, Kanuni na Mifumo ya
Udhibiti ya kuwezesha Nishati Safi ya Kupikia, Je ni mifumo ipi
huwezesha upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia,” amesema Makamba na
kuongeza,
“Sasa
kuna hatari ya mijadala hii kuwa na mitazamo tofauti ya kifalsafa na
kiitikadi (sio ya kisiasa). Kikubwa ni kupata njia ya tunapotaka kwenda.
Mwisho wa siku tunachotafuta ni njia na mkakati wa kufika tunapotaka
kwenda,”.
Ametumia
fursa hiyo kubainisha kuwa moja ya kazi ya kikosi kazi kitakachoundwa
ni kuja na njia na mkakati wa namna ya kufanikisha jambo hilo.
“Imani
ni kwamba kikosi kazi kije na njia na mkakati wa kwenda tunapotaka
kwenda (Kufikia Nishati Safi ya Kupikia),” amesisitiza Makamba.
Awali
akichokoza mada hiyo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine Prof. Romanus Ishengoma amesema Sera ya Nishati ya mwaka 2003 na
2015 zote zinalenga kuhama kwenda kwenye matumizi ya Nishati Safi ya
Kupikia.
Hata
hivyo Ishengoma amebainisha kwamba moja ya mapungufu ya Sera hiyo
haitoi ufafanuzi kwamba Nishati Safi ya kupikia ni ipi na kwamba
imeshindwa kutoa mwelekeo wa namna ya kufanikisha jambo hilo.
Hivyo ameshauri kwamba kama kuna uwezekano Sera hiyo ipitiwe upya au iungwe mkono kwa kanuni na sheria.
Vile
vile ameshauri kwamba ili kufikia lengo la Nishati Safi ya Kupikia kwa
kila mwananchi ni lazima kuwe na kipindi cha mpito kwani watu wa
vijijini hawawezi kumudu gaharama kwa sasa kutokana na vipato vyao.
Katika
hatua nyingine, amesema kuwa Serikali inawakaribisha wawekezaji wa
bidhaa ya nishati kuja kuwekeza nchini ili kuchochea upatikanaji wa
nishati safi na salama.







No comments:
Post a Comment