Wagombea 13 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba SC utakaofanyika Januari 29, mwakani.
Kati ya wagombea hao wanne wanawania nafasi ya mwenyekiti na tisa nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.
Miongoni mwa waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti ni aliyekuwa Mtunza Fedha wa klabu, Yusuph Nassor Majid ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS).
Wengine wanaowania ni Makamu Mwenyekiti wa zamani Geofrey Nyange ‘Kaburu’ Yusuph Omar Yenga, na Eng. Rashid Khamsini.
Katika nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi mpaka sasa waliochukua fomu ni wagombea tisa.
Wagombea hao ni Iddy Noor Kajuna, Abubakar Zebo, Eng. Rashid Khamsini, Hawa Subira Mwaifunga, Laurian Mganga, Elisony Edward Mweladzi, Lameck Lawrance na Abdallah Rashid Mgomba.
Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litafungwa rasmi Disemba 19, mwaka huu.
December 15, 2022
Home
Unlabelled
13 WACHUKUA FOMU SIMBA SC, WANNE WAUTAKA UENYEKITI
13 WACHUKUA FOMU SIMBA SC, WANNE WAUTAKA UENYEKITI
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment