HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 15, 2022

Chuo Kikuu Mzumbe chakaribisha wawekezaji


Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dk. Ali Shein (katikati) ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akiwa katika maandamano kuelekea katika eneo la mkusanyiko wa mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.
Mlau akiongoza maandamano.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dk. Ali Shein ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitangaza mkusanyiko kuwa mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe.
Baadhi ya wahitimu wakiwa katika mkusanyiko wa mahafali.

Kaimu Rasi Ndaki ya Dar es Salaam, Dk. Correta Komba.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dk. Ali Shein ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akimkabidhi cheti mwanafunzi bora Robinson Majaliwa katika mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, akionyesha cheti baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi.

Robinson Majaliwa ambaye aliibuka mwanafunzi bora katika mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, akionyesha cheti baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi.



Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dk. Ali Shein ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akipokea kitendea kazi 'kishkwambi' kutoka kwa Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha wakati wa mahafali ya 21 ya chuo hicho Ndaki ya Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dk. Ali Shein ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akimkabidhi kitendea kazi 'kishkwambi' Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Saida Yahya Othman.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dk. Ali Mohamed Shein akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa kitendea kazi na Makamu Mkuu wa chuo. 

 

Na Mwandishi Wetu

 

CHUO Kikuu Mzumbe Kimewakaribisha wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenda kuangalia fursa za uwekezaji zilizopo katika Chuo hicho.

Hayo yamesemwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hizo,   Profesa William Mwegoha wakati akizungumza katika Mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 15, 2022 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa  Chuo hicho kina wakaribisha wawekezaji wakaangalie namna ambavyo wanaweza kushirikiana kufanya shughuli za maendeleo. Ikiwa pamoja na kuanzisha miradi inayoweza kutekelezwa kwa ubia kwa mujibu wa miongozo ya Serikali.

Amesema kuwa bado kuna fursa nyingi ikiwa pamoja na ujenzi wa hosteli, Sehemu za biashara, Sehemu za Michezo pamoja na burudani.

Prof. Mwegoha amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe Kituo cha Tegeta bado kinauhitaji mkubwa wa mabweni kwa wanachuo wa Kituo hicho.

Amesema kuwa  Chuo hicho kinasera ya Uwekezaji ya 2020 ambayo inatoa fursa ya ubia na wawekezaji mbalimbali.

Kwa upande wa maendeleo ya kitaaluma ya Tehama Prof. Mwegoha amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe, wanashirikiana na taasisi mbalimbali za elimu  kwa kutengeneza Miundombinu.

Katika mahafali ya 21 ya Chuo hicho Wahitimu 240 wametunukiwa Shahada za Umahili katika Fani mbalimbali,  Kati ya hao wanawake ni 114 sawa na asilimia 47.5 na wanawake ni 126 sawa na asilimia 52.5 amesema idadi hiyo ya  wanawake imezidi kuongezeka kwa kila mwaka. 


No comments:

Post a Comment

Pages