HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 16, 2022

 Liwale wahimizwa kulinda amani


Mkuu wa Wilaya ya Liwale akizungumza katika mradi wa Mama na Mtoto. Wilayani Liwale uliohudhuliwa na madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama na watumishi wa halmashauri ya Wilaya hiyo.

Na Mwandishi wetu

MKUU wa Wilaya wa Liwale Bi, Judy Nguli amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuendelea kulinda amani na usalama wilayani humo ili kusaidia maendeleo ya nchi na kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha maisha ya wananchi.

Aliyasema hayo jana katika uzinduzi wa mradi wa kuboresha afya ya mama na mtoto wa miaka mitatu unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya na Shirika la Madaktari wasio na mipaka wilayani hapo.


“Mradi huu ni mkubwa na umekuja  na utakao  wamama na watoto katika wilaya yetu maana si rahisi kukuta huduma ya afya kwa urahisi kwa umbali uliopo kutokea Nalengwe  na Barikiwa, tumetunukiwa tunawashukuru,” alisema Nguli

Alisema mradi huo umekuja kwa wakati muafaka ambapo wananchi wana uhitaji wa kupata huduma bora za afya kama ilivyo katika ilani ya chama.

“Tuutunze mradi huu, tufanye kazi kwa bidii, tulinde amani na usalama ili hata wataalamu wanaoendelea kuja waweze kuongeza muda wa kufanya kazi  wilayani kwetu wakijua wanalindwa, “ alisema

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Liwale Bw. MOHAMED Mtesa, alisema mradi huo utatekelezwa kadiri ya makubaliano ili kuboresha huduma ya mama na mtoto wilayani hapo na kupunguza vifo vya uzazi na watoto chini ya miaka mitano.


 Aliwasihi watumishi wote kufanya kazi kwa pamoja wakishirikiana na wadau ili kupunguza kero kwa wananchi.


Naye Mratibu wa mradi huo wa shirika la Madaktari Wasio na Mipaka Bw. Jomah Kolie alisema lengo la mradi huo ni  kuboresha  rufaa za wagonjwa kutoka zahanati za vijijini kwenda vituo vya afya na hospitali za rufaa.


“Tutasaidia pia kongeza  baadhi ya madawa na vifaa tiba, tumeongeza watumishi wa afya 41 tutakaowalipa ili kukidhi mahitaji ya hospitali, zahanati na vituo vya afya,” alisema Jomah


Alisema mradi huo pia utachangia katika kupunguza vifo na maradhi kwa wajawazito na watoto chini ya miaka 5 katika hospitali ya halmsahauri na vituo vya afya  Mpengere na Kibutuka na Zahanati za Mlembwe, Kimambi na Barikiwa.

No comments:

Post a Comment

Pages