Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kwa
kuzingatia maono ya Mtukufu Aga Khan, ya kuwezesha huduma bora za afya
kupatikana kirahisi, Taasisi ya Utoaji Huduma za Afya ya Aga Khan,
Tanzania (AKHST) kupitia Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania (TCCP)
imenunua moja ya kifaa cha kisasa cha tiba ya mionzi na vifaa vingine
vinavyohusisha matibabu hayo vitakavyofungwa katika Kituo cha Huduma za
Saratani cha Aga Khan kilichopo Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam
(AKHD).
Hospitali
ya Aga Khan, Dar es Salaam itakuwa hospitali ya kwanza nchini Tanzania,
na ya pili Afrika Mashariki na Kati kuwa na vifaa vya teknolojia hiyo.
Kwamba
hii ineonesha kuwepo kwa maono na uvumbuzi unaolenga kusaidia wagonjwa
ambapo leo imeshuhudiwa utoaji huduma bora za afya nchini na pengine
katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, ukipata teknolojia bora zaidi ya
matibabu ya saratani, na kuifanya kuwa kituo mahususi cha matibabu ya
saratani Afrika Mashariki na Kati.
Akizungumza
katika hafla ya utiaji saini mkataba wa manunuzi wa vifaa hivyo jijini
Dar es Salaam Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya
Aga Khan Dar es Salaam na Meneja wa Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania
(TCC) Dkt. Harrison Chuwa amesema kifaa kitakachofungwa ni modeli mbili
za linear accelerator kuongeza kasi ya matibabu ya saratani kwa njia ya
mionzi.
Dkt.
Chuwa ameongeza kuwa “Kusainiwa kwa mkataba huu manunuzi na uwekaji wa
mashine ya mionzi unakifanya kituo cha matubabu ya saratani kuwa na
mashine za kisasa, ya kwanza na ya aina yake nchini na Kanda ya Afrika
Mashariki, ikiwezeshwa na CT simulator: Discovery TM RT kutoka kampuni
ya GE Healthcare na Wide-bore, teknolojia ya MaxFOV inayoruhusu
mwonekano kamili na sahihi, kingo-kwa-kingo, picha ya CT na teknolojia
ya MicroVoxel ambayo hutoa na kutupatia miundo midogo, kuwezesha njia
sahihi na kutoa DRR zenye mwonekano bora na usahihi wa picha,”.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Tiba na Afya, Mtandao wa Maendeleo wa Aga
Khan (AKDN), Dkt. Gijs Walvaren, amesema “ Lengo letu linabakia katika
kukuza ubora wa utoaji wa huduma za afya na usalama wa wagonjwa na
kuongezeka kwa upatikanaji kutoka huduma ya msingi hadi ngazi ya tatu/
juu kupitia uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikijumuisha vifaa,
teknolojia, wafanyakazi waliofunzwa vyema na wenye uwezo pamoja na
ithibati ya JCI ikifuatiwa na uidhinishaji ujao wa OECI, hizi zifuatazo
kituo cha huduma ya saratani cha Aga Khan (AK-CC) kuwa moja ya vituo vya
juu vya saratani barani Afrika na ulimwenguni,”.
Ameongeza
“Pili, kituo hicho kitasaidia juhudi za Serikali katika kupanua huduma
za matibabu ya saratani kwa Watanzania na kuongeza utalii wa kimatibabu
katika ukanza mzima,”.
Nae,
Makamu wa Rais, Huduma za Kimabara kutoka Elekta Feres Al Hasan amesema
Kampuni ya Elekta ina kusudi moja ambalo linawapatia motisha kama
kampuni na mtu binafsi.
“Matumaini
kwa kila mtu anayehusika au kuguswa na Saratani. Hili linatuongoza
kuelekea maono yetu ya kuwa ulimwengu ambapo kila mtu anaweza kupata
huduma bora ya matibabu ya saratani. Na tunapanga kufika huko kupitia
dhamira yetu ya kuboresha maisha ya wagonjwa kwa kufanya kazi pamoja na
wateja na washirika wetu,” amesema Al Hasan.
Kwamba
kama mvumbuzi mkuu wa tiba ya mionzi, kampuni ya Elekta imejitolea
kuhakikisha kwamba kila mgonjwa anapata huduma bora zaidi ya saratani
kadri iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment