Kampuni
ya Usambazaji wa Gesi Majumbani ya Taifa Gas imetoa msaada wa mitungi
ya gesi 150 kwa Baba na Mama Lishe wa Kisutu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
jijini humo wakati wa hafla ya kukabidhi kwa mitungi hiyo Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Ngw’ilabuzu Ludigija amempongeza Mbunge wa Jimbo la
Ilala ambaye pia ni Naibu Spika Mussa Zungu kwa kushitikiana na Taifa
GAS kutoa msaada huo.
Amesema
gesi hiyo ni salama kwa matumizi kwani inasaidia katika utunzaji wa
mazingira na kwamba wana gesi ya kutosha kwa matumizi ya nchi nzima
“Hongereni
kwa kazi nzuri ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za
kuhimiza matumizi ya nishati mbadala, hivyo mama lishe na baba lishe
haya ni matunda ya maelekezo ya Rais,” amesema Ludigija na kuongeza,
“Hivyo nyie ndiyo wakwanza kula matunda haya ya kuwekwa pamoja mahali rasmi pa kufanyia shughuli zenu,”.
Hivyo
Ludigija amewataka baba na mama lishe hao kuwa mabalozi kwa wemgine
kuwaeleza kiacha kipikia barabarani kwani kufanya hivyo kuna haribu
miundombinu ya barabara.
Ametumia fursa hiyo kuwataka wana Ilala kuhakikisha wanaitikia witu wakufanya shughuli zao katika maeneo rasmi.
Akizungumzia gesi hiyo, amesema kwamba ni salama na itawasaidia kiwaondolea matatizo mbalimbali yakiwemo ya kiafya na mazingira.
Ameelza
kwamba Taifa GAS kwa sasa imesambaa nchi nzima, hivyo ameipongeza
kampuni hiyo kwa kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuhimiza matumizi
ya nishati mbadala ambayo inasaidia kuepusha Taifa kuingia katika hali
ya jangwa.
Kwani jambo hilo litasaidia kuokoa misitu kukatwa kwa matumizi ya kuni na mkaa.
Kwa
upande wake, Naibu Spika Zungu, amesema kwamba wamesaidia mitungi hiyo
kwa sababu baba na mama lishe wamekuwa wakihangaika na moshi kutokana na
kutumia mkaa na kuni.
Aidha
amesema kwamba baada ya kukaa nao hivi karibuni waliona ni bora
kuwasaidia ili waweze kutumia nishati mbadala badala ya mkaa na kuni.
Naibu
Spika Zungu amesema kwamba kutokana na matumizi ya nishati ya kuni na
mkaa, takribani viwanja milioni moja vya mpira vyenye misitu vimekuwa
vikiharibiwa hali inayosababisha nchi kuingia katika jangwa.
“Tumekaa
na Taifa GAS kuwaomba, hivyo mitungi hii 150 inatolewa bure, lakini
sharti yake gesi ikiisha utanunua kwa yule aliyekupatia, ukinunua
kwingine sio uungwana,” amesema Zungu.
Zungu amewataka kutokuendelea kutumia mkaa na kuni kwani kutumia nishati hizo ni kuliumiza Taifa kwa kuliingiza kwenye ukame.
Nae,
Meneja wa Mahusiano Mema kutoka Taifa GAS, Angel Mwita, amesema wametoa
msaada wa mitungi hiyo kwa kushirikiana na Mbunge wa Ilala ikiwa ni
sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuhimiza matumizi ya
nishati mbadala.
No comments:
Post a Comment