HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 04, 2023

BURIANI BENEDIKTI XVI

Adeladius Makwega-CHAWA

 

“Mtumishi wa umma wa ngazi ya kati, Mkatoliki,Hajaoa, Mwenye umri wa miaka 43, mtu mwema, Raia, Anatafuta mwanamke wa kuoa, Awe Mkatoliki, Mwanamke mwaminifu , Awe anajua kupika, Awe anaweza kuzifanya kazi zote za nyumbani kikamilifu, Awe na ujuzi wa kushona nguo, Awe ma malengo ya kuolewa, Awe na matamanio lakini siyo kabla ya ndoa.” 


Haya yalikuwa maelezo ya jarida la kila wiki la Kanisa Katoliki la
Liebfraubote juu ya askari polisi aliyekuwa akisaka mchumba wa kuoa.

 

Maria Peintner, mwanamke wa Kijerumani, mwenye miaka 36, binti wa muoka mikate aliyesomea upishi alichangamkia fursa hiyo na baada ya miezi minne mwaka 1920 walioana na mwaname aliyenadi hayo.

 

Katika ndoa yao Maria na Joseph walizaa watoto watatu Maria (1921), Georg (1924) na Joseph (1927). Huku jina la mtoto wa kwanza na jina la mtoto wa mwisho yakiwa majina ya wazazi hao.

 

Huyu mtoto wa mwisho Joseph ndiyo Baba Mtakatifu Benedikt wa XVI ambaye jina lake halisi ni Joseph Alois Ratzinger aliyefariki dunia Disemba 31, 2022 huko Vatikani ambapo katika uhai wake aliwahi kushika nafasi kadhaa kubwa katika Kanisa Katoliki Ulimwenguni kama vile Askofu wa Roma na Mkuu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni tangu mwaka 2005-2013 alipojiuzulu nyadhifa hizo.


Akiwa Baba Mtakaffu alijiuzulu kama ilivyokuwa kwa Baba Mtakafifu Gregori XII mwaka 1415 miaka zaidi ya 600 iliyopita.

 

Mara baada ya kufariki dunia kiongozi huyu aliyewahi kuliongoza Kanisa hilo lenye waamini zaidi ya Bilioni moja Ulimwenguni anakumbukwa kwa mambo mengi.Mojawapo ni kisa hiki kilichosimulia baada ya Baba Mtakatifu Benedikt XVI enzi ya uhai wake mwaka 2006 alipotembelea eneo la Bavaria Kijiji cha Marktl am Inn Ujerumani alipokwenda kuzulu makaburi ya wazazi wake. Alishangazwa baada ya kubaini kuwa baba na mama yake yaani Joseph na Maria Ratzinger walikutana kwa mara ya kwanza katika tangazo la kutafuta wachumba ambapo Joseph Ratzinger alipojitangaza katika jarida la kila wiki la Kanisa Katoliki la Liebfraubote mwaka 1920. Ikiwa ni miaka 86 baada ya tukio hilo.

 

Maria Peintner mama wa Baba Mtakatifu Benedikt wa XVI alipoona tangazo hilo alichangamkia fursa na kuolewa na afande Joseph Ratzinger, mama huyu hakuyafahamu ya kesho kuwa atazaa mtoto wake wa mwisho ambaye atakuja kuwa Baba Mtakatifu.

 

Hayo ndiyo maisha yalivyo, hakuna anayeifahamu kesho.

 

Je msomaji wangu unafahamu wazazi wako kipi kiliwakutanisha?

 

Wakati Vatikani inamzika Baba Mtakatifu Benedikt wa XVI mimi na wewe tutafakari hilo la ndoa hiyo ndani yake aliyepozaliwa kiongozi huyu.

 

Wazazi wako walikutana wapi? Wewe na mumeo mmekutana wapi kwa mara ya kwanza?

 

Mwanakwetu anasema BURIANI BENEDIKT XVI.

 

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

No comments:

Post a Comment

Pages