HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 10, 2023

MO DEWJ ATETA NA WACHEZAJI DUBAI, AMTAKIA KWAHERI BARBARA GONZALEZ

Na John Richard Marwa



Rais wa heshima na Mwekezaji wa Klabu ya Simba Mohamed Dewji 'Mo' amezungumza na wachezaji na benchi la Ufundi la klabu hiyo katika kambi yao aliyowawekea ughaibuni.




Simba wametimiza siku tatu tangu watimkie Dubai kwa kambi ya wiki moja ikiwa ni kufuatia mualiko Bilionea huyo kijana Barani Afrika.


Mo ametinga kambini na kuzungumza na wachezaji, benchi la Ufundi na sehemu ya viongozi waliombanata na kikosi hicho, amewataka wachezaji kujituma zaidi ili kufikia malengo ya klabu iliyojiwekea kwa msimu huu.


Katika hatua nyingine amewashukuru wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wanaomaliza muda wao huku akiwatakia heri wanachama kuelekea Mkutano Mkuu wa klabu hiyo.


"Shukrani kwa wadhamini, mwenyekiti wa Bodi nifanya nae kazi kwa karibu, na niwatakie kila la heri wajumbe wanaomaliza muda wao na pia  nawatakia wananchama Mkutano Mkuu mwema na  Shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea kuisapoti timu yetu." amesema Mo Dewji.


SHUKRANI NA KILA LA HERI KWA BARBARA GONZALEZ


Pia Bilionea Mohamed Dewji 'Mo' amemshukuru na kumtakia kila la heri Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba anayemaliza muda wake Bi Barbara Gonzalez kwa kumshukuru kwa utendaji wake uliotukuka.


"Kipekeee nimshukuru CEO ambaye amemaliza muda wake ndani ya Simba Bi Barbara Gonzalez, Barbara alikuwa msaidizi wangu baadae akawa CEO wa Simba.


"Namshukuru sana, amejitolea kwa hali na mali kuisaidia ifike mbali zaidi. Mimi kama Mohamed kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, wanachama, mashabiki na wachezaji tunamtakia kila la heri katika maisha yake mapya." amesema Mo Dewji'Mo'

No comments:

Post a Comment

Pages