Na John Richard Marwa
Yawezekana isiwe ilivyotarajiwa leo katika Dimba la Amani pale Zanzibar kuzitazama Simba na Yanga zikimenyana ama mmoja wao akizichapa na Azam FC kusaka mwali wa Kombe la Mapinduzi makala ya 17.
Story ni tifauti sana kwa sababu visiwa vya marashi ya karufuu vina bashasha kwelikweli wanapoenda kushuhudia Mlandege wakiandika historia ya kusaka heshim ya Zanzibar katika fainali hizo ya kucheza fainali tangu mwaka 2012.
Ni Fainal ya heshima kwa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ikiwa imetimia miaka 59 na jana ndo kilikuwa kilele chake.
Leo ni sherehe za kimichezo ambazo zinahitimisha sherehe za miaka 59 kwa Fainali kati ya Mlandege FC dhidi ya Singida Big Stars mtanange huo unatarajiwa kuanza majira ya 20:15 huku shamrashamra zikitarajiwa kuanza majira ya saa 18:00 jioni.
Kuelekea mchezo wa leo Singida Big Stars hesabu zao zote ni kuondoka na Kombe hilo.
Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hans Pluijm imetinga hatua hiyo kwa kuichapa mabao 4-1 Azam FC.
Mtupiaji wa mabao yote ya Singida Big Stars ni Francy Kazadi ambaye kibindoni anafikisha mabao matano akisimama kwenye kilele cha ufungaji bora katika fainali hizo.
Mlandege nao waliwatungua Simba kwenye hatua ya makundi na kuwavua ubingwa kisha kuiondosha Namungo FC katika hatua ya Nusu Fainali kwa mikwaju ya penati (5-4) baada ya sare ya bao (1-1) katika dakika 90.
No comments:
Post a Comment