HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 12, 2023

 Walinda amani kutoka Tanzania watoa dawa, matibabu kwa wananchi Kijiji cha Potopoto Afrika ya Kati  

Mwananchi wa kijiji cha Potopoto Afrika ya Kati akipatiwa matibabu.

Mgaga Mkuu wa Kikosi cha TANBAT6 akikabidhi dawa za kutibu binadamu katika Zahanati ya Potopoto iliyopo Mambele kadei Afrika ya Kati.

 

Na Mwandishi Wetu


KIKOSI cha sita cha Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania (TANBAT 6) wametoa msaada wa dawa na matibabu katika Zahanati ya Potopoto iliyopo katika kijiji cha Potopoto wilaya ya Mambele Kadei Afrika ya Kati.


Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa habari wa kikosi hicho Kapteni Mwijage Inyoma alisema mkuu wa kikosi hicho cha sita, Luteni Kanali Amini Mshana aliungana na walinda amani hao kutoa matibabu katika Zahanati hiyo ya Potopoto.


Inyoma alisema utoaji wa dawa na

matibabu  hayo umekuwa na mwitiko mkubwa kutoka kwa wananchi wa Kijiji hicho  ambao wametoa shukrani kwa Umoja wa Mataifa (UN) na walinda amani hao kutoka Tanzania kwa msaada huo.


Wakitoa shukurani zao wenanchi wa Afrika ya kati walisema kuwa Tanzania na wanajeshi wake wana upendo kwao kwani tangu waanze  jukumu la ulinzi wa amani wamepata misaada mingi kwao.


"Jeshi la walinzi wa amani kutoka Tanzania wametusaidia mambo mengi, tunasema asante kwa kutoa matibabu, maana wananchi waliyo wengi hawana uwezo wa kununua dawa lakini Tanzania  pamoja na majukumu  yake ya ulinzi wa amani wanasaidia dawa huu ni upendo na moyo wa upendo kwa  Afrika ya kati."


Naye Mganga wa Zahanati ya Potopoto Dk. alitoa shukurani zake  baada ya kuupokea dawa hizo akisema


"Tunashukuru sana kwa kupatiwa dawa hizi ambazo zitasaidia kutoa matibabu kwa wananchi wetu lakini pia tunashukuru kwa kutoa matibabu kwa wagonjwa waliopo hapa kwenye Zahanati, Walinda Amani wa Tanzania mnazidi kutupa upendo na ushirikiano mkubwa katika suala la kutunza afya za wananchi wa Afrika ya kati nikiwemo hata Mimi," alisema

No comments:

Post a Comment

Pages