HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 23, 2023

Takukuru yatakiwa kuchunguza tuhuma za rushwa kwa Majaji na Mahakimu

Kufuatia tuhuma za rushwa kwa baadhi ya majaji na mahakimu, zilizotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mkoani humo, Dk. Rashid Chuachua, Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu Mustapher Mohamed Siyani ametaka tuhuma hizo zichunguzwe na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

 Jana Januari 22 wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya sheria mkoani humo, Dk. Chuachua alinukuliwa akisema kuna baadhi ya majaji na mahakimu wanajihusisha na vitendo ya ukiukaji wa maadili kwa kupokea rushwa kwa njia ya miamala ya simu.

Baada ya tuhuma hizo, Jaji kiongozi Siyani amemuagiza Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Rose Ebrahim kuwasilisha hoja hiyo kwa uongozi wa Takukuru wa mkoa huo ili kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo na kubaini ukweli.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 23 na mkuu wa kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Artemony Vicent imesema;

“Ikithibitika pasipo na shaka kwamba tuhuma hizo zina ushahidi wa kutosha bila ya kuathiri hatua nyingine zitakazochukuliwa na vyombo husika, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watumishi watakaothibitika kutenda kosa hilo.

"Ni matumaini ya uongozi wa mahakama kwamba waliotoa tuhuma watakuwa tayari kuthibitisha ili sheria ichukuae mkondo wake bila kumuonea yeyote au kuchafua taswira ya muhimili wa mahakama na watumishi wake," imeeleza taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages