HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 04, 2023

UWT YAMPONGEZA RAIS DKT SAMIA SULUHU KWA KUIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI


 

MWENYEKITI  wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini


Na Oscar Assenga,TANGA


MWENYEKITI  wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda amesema UWT imekoshwa na uamuzi wa kihistoria wa Rais Dkt. Samia Suluhu  kuondoa  zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini maamuzi ambayo yameleta faraja kwa vyama hivyo na hivyo kufungua ukurasa mpya wa demokrasia nchini.

Chatanda  aliyasema hayo leo kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Tanga wakati akizungumza  na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu kuondoa zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa nchini ambapo.

Alisema  kwamba UWT imekoshwa na hatua ya kihistoria kuondoa zuio la mkutano ya hadhara vyama vya siasa ikiwemo kukwamua mchakato wa kupata Katiba mpya ambapo alisema  kwamba wao wanaunga mkono uamuzi wa Kukwamua mchakato wa  marekebisho ya Katiba  ya Tanzania  na hivyo tunahimiza amani na utulivu wakati wote wa kusubiri Serikali kukamilisha taratibu zote za kuanza mchakato huu kama alivyoeleza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika  hotuba yake jana tarehe 3 Januari 2023.

Alisema  pamoja na kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ili kupanua wigo wa demokrasia nchini ambapo alisema maamuzi ya Rais Dkt Samia yameleta faraja kwa vyama mbalimbali vya siasa nchini na kuwezesha kufikia hatu kubwa ya kidemokrasia nchini.

Aidha  alisema Rais Dkt Samia ameendelea kuonyesha udhabiti wa kauli zake kwa matendo ambapo hata alipohutubia Taifa mara baada ya kuapishwa Maci 19,2022 alisema wakati huo sio wa kutazama mbele kwa mashaka bali ni kwa  kutazama kwa matumaini mwisho wa kumnukuu.

Mwenyekiti  Chatanda alisema maamuzi aliyoyafikia Rais Dkt Samia kupitia mchakato wa maridhiano kuanzia kuundwa Kikosi cha kazi pia mazungumzo kati ya Vyama vya Siasa na Vyama vya CCM na Chadema yameleta matumaini mapya katika kujenga demokrasia ya kuaminiana baina ya vyama vyote vya siasa nchini ambayo ni chachu katika ujenzi wa Taifa lenye umoja Amani a Utulivu.

“Lakini  niwaambie kwanza falsafaya Rais Samia Suluhu ni kujenga upya nchi yenye  umoja katika ujenzi wa Taifa inayoongozwa falsafa ya 4R maridhiano ustahimilivu,mabadiliko na kujenga upya nchi hadi sasa falsafa hiyo imefanikiwa kwa asilimia 100” Alisema Chatanda.

Hata  hivyo alisema sio tu kwa kuleta mafanikio makubwa ya kisekta aliyotekeleza Rais kwa muda mfupi wa chini ya miaka miwili madarakani licha kuipokea nchini ikiwa na hali tete ya kutokana majanga ya Corona ,vita ya Ukraine na kufiwa na mtangulizi wake mwaka 2021.

“Kwa  kweli sisi UWT tunasema Rais Dkt Samia amefanya jambo kubwa sana hivyo tunampongeza na hizo zinazotokana na matokeo  ya mkutano baina ya  Rais Samia na vyama vya siasa kwenye usajili wa kudumisha nchini,uwt wanampjgeza  Rais Samia kwa kufanya maamuzi yalitileta furaha isiyo na kifani kwa wananchi wa Tanzania na wapenda Amani dunia kote kwa kutoa majawabu ya vikwazo vya demokrasia nchini wao na  majanga ya korona,vita  ya Ukraine na kufiwa na mtangulizi wake Mwaka 2021" Alisema Chatanda.
 
Aliongeza  kwamba bali falsafsa hìzo zinahimiza siasa za kustaarabu zenye kuweka watu pamoja,kujenga hoja za ushawishi kupitia majadiliano mazungumzo kuhusisha vyama vya siasa katika kuendesha nchi hivyo kutokana na hilo UWT wanampongeza Rais huku wakieleza kwamba hakika wanawake wanaweza.

Hata  hivyo alisema kwamba Jumuiya hiyo ya UWT inawahimiza viongozi wanawake wa vyama mbalimbali kuandaa mikutano mingi ya hadhara ili kuweza kupokea  changamoto mbalimbali zinazowagusa wanawake wa Tanzania wanakabiliwa na  changamoto zinazofanana bila kujali itikadi zao na pia katika mikutano wanapendeleza hatua mahususi za kuchukua kwa Serikali ili kumkomboa mwanamke kiuchumi,kijamii na kisiasa.

Mwenyekiti  Chatanda alisema kwamba pia wamefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya awamu ya sita ya kuridhia mapendekezo ya kikosi kazi cha kufanya marekebisho ya sheria kadhaa ndani ya nchi kwa nia ya kuimarisha demokrasia zaidi ambayo yatahusisha wananchi.

Alisema  wanaamini marekebisho hayo pia yatazingatia masuala ya usawa wa kijinsia katika kuongeza uwakilishi wa wanawake kwenye siasa na uongozi kuanzia kwenye vyama vya siasa kama ambayo wameshuhudia namna Rais Samia  Suluhu alivyojitahidi kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye uongozi ndani ya Serikali yake na chama cha Mapinduzi.


Mwenyekiti  Chatanda aliwahimiza viongozi wake wa Jumuiya ya UWT kuanzia ngazi za tawi, kata/wadi, Jimbo, wilaya, mkoa mpaka Taifa pamoja na madiwani, wawakilishi na wabunge wanawake kufanya mikutano ya hadhara kwa  kufuata taratibu zote ,mikutano hiyo ilenge kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 , kusikiliza kero za wananchi na kujibu hoja mbalimbali zitakazopotoshwa kwa lugha ya kistaarabu na kwa kutumia takwimu sahihi, sisi Viongozi wa UWT Taifa tutaonyesha mfano kwa kutumia fursa hii iliyotolewa na Mhe Dk Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
 
Hata  hivyo pia alitumia nafasi hiyo kuitaka Jumuiya ya UWT kuendelea kuwaomba Watanzania kuendelea kumuamini Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumuunga mkono kwani ana dhamira njema ya kujenga Taifa  linaloongea lugha moja, na ambalo kila mmoja anashiriki katika ujenzi wa Taifa lake.

No comments:

Post a Comment

Pages