Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Baada
ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan
kutangaza kuruhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa
nchini,Vyama mbalimbali vya siasa vimejitokeza na kupongeza hatua hiyo.
Wakizungumza
na waandishi jijini Dar es salaam viongozi wakuu wa vyama hivyo
wamesema hatua hiyo ya Rais Dkt. Samia ni ya kupongezwa na ni muhimu kwa
maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumza
katika mkutano huo,Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Cuf, Profesa
Ibrahim Lipumba amesema kuwa kauli ya Rais Samia imeleta matumaini
makubwa kwa siasa za Tanzania na imeonyesha ni jinsi gani ana maono ya
kukuza mashirikiano nchini.
Nae,
Mwenyekiti wa Chama cha ADC,Hamad Rashid amesema kuwa tukio hilo kwa
viongozi wa vyama vya siasa ni la kihistoria na limeleta fursa kwa
wananchi sasa kuweza kusikiliza sera za vyama vya siasa na kuchagua
viongozi wao ambao wameridhishwa na sera zao.
Ameongeza
kuwa Rais Dkt Samia ametembea katika kiapo chake na anafaa kuungwa
mkono na kila mwenye kutambua thamani ya demokrasia.
Hata hivyo Hamad Rashidi amewataka wanasiasa kutumia fursa hiyo kwa kuzingatia sheria na bila kuleta uvunjifu wa amani.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa amesema kuna kila
sababu ya kumpongeza Rais Dkt Samia kwa kuonyesha uzalendo mkubwa kwa
kuzungumza na vyama vyote kikiwemo Chama cha demokrasia na maendeleo
(Chadema)kupitia mwenyekiti wao,Freeman Mbowe.
"Hii
ndiyo Tanzania tunayoitaka,tukae pamoja,tubishane pamoja na Hii ni
sababu kubwa ya kumpongeza Rais na baraza la vyama vya siasa litampa
ushirikiano mkubwa na kumuunga mkono bila kuangalia itikadi za vyama
vyao"alisema.
Nae, Joseph
Selasini wa Chama cha NCCR Mageuzi amesema maamuzi ya jana ni maamuzi
mazito sana kufanywa na Rais ambaye naye chama chake kiko kwenye
ushindani kisiasa hivyo ni ya kuungwa mkono.
Ameongeza kuwa sasa wanasiasa watamsaidia Rais kwa kuwasema na kuwakemea wote wanaolihujumu Taifa wakiwemo wala rushwa.
No comments:
Post a Comment