HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 17, 2023

ROBERTINHO AWAONYA RAJA CASABLANCA

Na John Richard Marwa


Wakati yakiwa yamesalia masaa kadhaa kuelekea mchezo wa pili wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL, kundi C, Simba SC wakiwaalika Raja Casablanca Kocha Mkuu wa Simba Mbrazil Robert Oliveira 'Robertinho' amewaonya wapinzani wake.



Simba wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukizi ya kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Horoya ya Guinea kwa bao moja kwa bila huku wapinzani wao wakiingia na kumbukumbu ya ushidi wa mabao matano kwa kalayi dhidi ya Vipers ya Uganda.


Ni mchezo wa kwanza wa Simba msimu huu hatua hiyo ya makundi msimu huu kucheza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa sehemu waliyoigeuza kuwa jehanu ya timu pinzani Barani Afrika.


Akizungumza leo kuelekea mchezo huo Kocha Robertinho amesema licha ya historia nzuri waliyonayo wababe hao kutoka Morocco mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wa nyakati hivyo hakuna kisichowezekana  mbele yao.


"Raja wana historia nzuri katika soka la Afrika lakini mpira wa miguu ni mchezo wa wakati, na kwa wakati huu mimi siangalii ukubwawao nina wachezaji wenye vipaji vikubwa sana na nina waandaa kushinda"


"Timu yangu lazima icheze mchezo mzuri na nimewaandaa kwa hilo kwa sababu kabla ya kufunga lazima ucheze mpira mzuri" amesema 

Robertinho.


Ikumbukwe kuwa Simba katika misimj ya hivi karibuni hawaja poteza mchezo wowote wa hatua ya makundi katika mashindano ya Klabu Barani Afrika.


Kuanzia msimu wa 2018/19 hadi msimu 2021/22 wameshiriki hatua ya makundi katika misimu mitatu na kuibuka na ushindi wa asilimia 100. 


Katika msimu hiyo mitatu Simba wamecheza michezo tisa kwa ujumla huku wakishinda yote bila hata ya sare wala suluhu.


February 18, 2023 Mnyama Simba anashuka dimbani kuandikisha rekodi nyingine ya msimu wa nne katika hatua ya makundi. Swali ni je, rekodi itaendelea pale kwa Mkapa na kauli mbiu ya ' KWA MKAPA HATOKI MTU '. Raja Casablanca watatoka ? 

No comments:

Post a Comment

Pages