Na Mwandishi Wetu
Baada ya kupitia nyakati ngumu za kupoteza michezo miwili mtawalia ya hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL, Leo Mnyama anashuka dimbani kwenye muendelezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania NBC PL dhidi ya Azam FC kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.
Simba wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na maumivu makali ya kupoteza mchezo dhidi ya Raja Casablanca kwenye kiota chao ambacho kilikuwa ni kaburi la timu kubwa kufungwa, jambo ambalo limewavuruga sana.
Simba wataingia kwenye mchezo wa leo wakihitaji matokeo chanya pekee ikiwa mchezo wa raundi ya kwanza walipoteza kwa bao moja mtungi dhidi ya hao matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC.
Kuelekea mchezo wa leo Kocha Mkuu Robert Oliveira amesema utakuwa mchezo mgumu na mzuri licha ya presha kubwa wanayokumbana nayo baada ya kupoteza michezo miwili dhidi ya Horoya na Raja Casablanca.
"Utakuwa mchezo mgumu na mzuri, vijana wangu wako tayari kwa ajili ya mechi hii na hii ni derby ambayo haiwezi kuwa rahisi." amesema Robertinho
Wakati Simba wakitoka kupoteza michezo miwili Azam FC wao wamekuwa nje ya mashindano kwa wiki mbili bila mechi ya kimashindano jambo ambalo linaongeza ugumu wa mchezo husika kwa timu zote mbili.
No comments:
Post a Comment