HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 20, 2023

TIMU YA TAIFA NYIKA KUREJEA JUMATANO

NA TULLO CHAMBO, RT

TIMU ya Taifa ya Mbio za Nyika iliyoshiriki mashindano ya Dunia huko Australia, inatarajiwa kurejea nchini Jumatano alfajiri, Februari 22, 2023.



Mashindano ya Nyika ya Dunia 'World Cross Country Championship', yalifanyika katika mji wa Bathurst, Australia na kushuhudiwa timu ya Tanzania ikikamata nafasi ya nane kwa upande wa wanaume 'senior'.


Timu hiyo ilikuwa ikiundwa na Josephat Gisemo ambaye alikamata nafasi ya 28, Inyasi Sulley 49, Fabian Sulle 52 na Mathayo Sombi 56 chini ya Kocha Denis Malle na Kiongozi wa msafara Wakili Jackson Ndaweka.


Kwa mujibu wa Wakili Ndaweka, msafara umeanza safari ya kurejea nchini ikitumia ndege ya Etihad.


"Vijana wamepambana kuipambania nchi na matokeo ndio hayo, tunarejea nyumbani kujipanga kwa mashindano mengine yanayotukabili, naomba Watanzania tuzidi kushikamana na kuwekeza kwenye timu zetu za Taifa," amesema Wakili Ndaweka na kuongeza.


Timu inatarajiwa kuwasili nchini Jumatano Februari 22 saa nane usiku Uwanja wa Kimataifa wa Julias Nyerere.


Baada ya mashindano hayo ya Nyika ya Dunia, Tanzania inakabiliwa na Mashindano ya Vijana Afrika Mashariki chini ya miaka 18 na 20 (EAAR U 18, U 20), ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji, Machi    10-11 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages