HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 19, 2023

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAVUTIWA NA MAENDELEO YA UJENZI BRT II

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya wajumbe wa kamati hiyo kukagua maendeleo ya mradi wa BRT II jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea mradi wa BRT II unaosimamiwa na TANROADS jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila (kushoto) akiteta jambo na mmoja wa wabunge mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea BRT II.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mama Anne Kilango Malecela akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kamatihiyo ilipokagua maendeleo ya mradi wa BRT II. 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa miundombinu ya BRT II kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea Makao Makuu ya TANROADS jijini Dar es Salaam.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya miundombinu inayosimamiwa na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), na kuitaka taasisi hiyo kuwasimamia kikamilifu wakandarasi ili waweze kukamilisha kazi zao kwa wakati.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso alipokuwa akitembelea na kushuhudia maendeleo ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka awamu ya pili, 'BRT II' ambao umeanzia Makutano ya Barabara ya Bandari hadi Mbagala ilipo Karakana ya Mabasi hayo.

Mhe. Kakoso amepongeza ujenzi wa barabara za juu katika mradi huo kwani umejengwa vizuri hivyo kuishauri TANROADS kuhakikisha maendeo ya chini ya madaraja hayo yaliowazi yajengewe uzio ili wananchi wasiyatumie vibaya kwani kwa sasa yapo wazi. 

"...Nimefuraishwa sana na barabara za juu ulizojenga katika mradi huu, lakini nashauri maeneo yale ya chini myajengee uzio ili yasibaki wazi kwani baadhi ya wananchi wanaweza kuyatumia vibaya," alisema Mhe. Kakoso. 

Kwa uapande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kutembelea mradi huo, alisema wizara yake imepokea ushauri na maelekezo ya wajumbe wa kamati hiyo na utahakikisha unayafanyia kazi yote.

Awali akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa miundombinu ya BRT II kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya BUNGE ya Miundombinu ilipotembelea Makao Makuu ya TANROADS, Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Eng. Rogatus Mativila alisema hadi sasa ujenzi wa BRT II umefikia asilimia 89.9 ukilinganisha na asilimia 50.1 kipindi kama hiki mwaka jana wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo.

"...Awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu inahusisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 20.3 kutoka katikati ya jiji hadi Mbagala; barabara za juu mbili, daraja moja juu ya reli, daraja moja la waenda kwa miguu, karakana moja na vituo vya mabasi," alisema Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Eng. Rogatus Mativila.

No comments:

Post a Comment

Pages