HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 13, 2023

NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA AWAPONGEZA TWCC KUANDAA VEMA USIKU WA TUZO KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI NA WENYE VIWANDA


Naibu Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, akimkabidhi tuzo Mhandisi  Debora Sengati ambaye pia ni Katibu wa Chama Cha Wahandisi Wanawake nchini.


 

Na Khadija Kalili

 

NAIBU Waziri wa  Wizara ya Uwekezaji  Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe amewapongeza wanawake wajasiriamali na wenye viwanda nchini kutokana na namna walivyo vinara katika kujituma kujikomboa kiuchumi na kuchangia katika kukuza pato na uchumi wa nchi.

Amesema hayo  katika hafla ya utoaji wa tuzo za Viwanda na Biashara iliyofanyika kwa msimu wa  tatu huku ikienda sambamba kwa kutanguliwa na  maonesho ya bidhaa za wanawake wenye viwanda nchini hafla hiyo  ilimefanyika Machi 11 usiku kwenye  Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Es Salam na  kuandaliwa na Chama Cha Wanawake Wafanyabiasha Tanzania (TWCC).

"Kundi la Wanawake wamekuwa wakijishughulisha katika shughuli mbalimbali za ubunifu wa bidhaa za Viwanda na kuleta tija kwa taifa na hasa ukimsaidia mwanamke kiuchumi umesaidia familia nzima" amesema Mheshimiwa Naibu Waziri wa Uwekezaji  Viwanda   na Biashara Kigahe.

Amesema kuwa   kinamama wanaongoza katika uchukuaji wa mikopo na kufanya jitihada za urejeshaji nchini kuliko makundi mengine ya wanaume na Vijana hivyo amesema serikali itaendelea kuwaweezesha kwa kuwapa mikopo kundi hilo  muhimu katika jamii.

Amesema kuwa amejionea hayo alipotembelea mabanda ya wajasiriamali na wafanyabiashara  kwenye viwanja vya Mlimani City na kwamba  ameona bidhaa  zenye  ubora na viwango vinavyokidhi  vigezo vya kitaifa  na kimataifa  hivyo hana budi kuwapongeza .

"Binafsi nachukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwani  ameifungua nchi  katika sekta ya uwekezaji  na kuboresha mahusiano yetu na nchi za nje kuvutia wawekezaji na kuongeza  mapato ya serikali kupitia uwekezaji.

"Nawapongeza sana TWCC kwani mmeonesha  ufanisi mkubwa  wa  kukuza  uchumi wa wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara hivyo serikali itaendelea  kuthamini mchango wenu  katika kukuza  uchumi  kwa wanawake  pia nawapongeza wanawake  wote nchini Tanzania kwa kujikomboa  kiuchumi  na kuchangia pato la taifa hivyo tunaahidi kuwa serikali itaboresha miundombinu  yenu  ya biashara" alisema   Mheshimiwa Kigahe.

Amesema mwanamke ni nguzo  imara ya familia hivyo ukimuwezesha mwanamke umefanya jambo kubwa kwenye familia serikali itaendelea kuhakikisha biashara za wanawake zinakua na zinaendelea kuleta tija kwa familia na Taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa TWCC Mwajuma Hamza amesema kuwa wajasiriamali  waliopatawa tuzo hizo ikawe chachu kwa wengine katika miaka ijayo.

"Tuzo hizi zikawe chachu ya kuwahamasisha na kuleta ushindani wa kibiashara ili mwakani kuwe na ushindani mkubwa"amesema Mheshimiwa Naibu Waziri huyo wa Viwanda na Biashara Kigahe.

Hafla hiyo imeandaliwa na TWCC na kudhaminiwa na Taasisi mbalimbali ambazo ni za binafsi na serikali baadhi uake ni  Giz, TPSF, UN WOMAN, TGNP, CLOUDS GROUP, UMOJA WA ULAYA, AZANIA BANK,EQUITY BANK na wengineo.

No comments:

Post a Comment

Pages