Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert John Chalamila akizungumzia mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita iliyolenga kumpongeza Rais Dkt Samia kwa kipindi cha miaka miwili tangu aingie Madarakani.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert John Chalamila amesema kuwa kazi ya Rais Dkt Samia haipaswi kupingwa au kubezwa kwa aina yoyote ile kutokana na kuonyesha mapenzi mema kwa wana Kagera na Watanzania kwa ujumla kutokana na ukomavu shupavu kisiasa katika ukamilishaji wa Miradi mikubwa kimkakati.
Chalamila ametoa kauli hiyo katika hafla ya uwasilishaji wa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita iliyolenga kumpongeza Rais Dkt Samia kwa kutimiza miaka miwili tangu aingie Madarakani iliyofanyika Machi 16,2023 katika Uwanja wa Mashujaa(Mayunga) uliopo Manispaa ya Bukoba Mkoani humo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa tangu Rais Samia alipoingia Madarakani mwaka 2021 alisikia kilio cha wazazi wengi waliokuwa wakililia kuchangishwa michango mingi ya kujenga madarasa karibu kila kipindi cha mwezi Januari, Novemba na Desemba ambapo baada ya hapo madarasa 881 yenye thamani ya sh. Bilioni 17 yalijengwa kwa awamu ya kwanza na kwa awamu ya pili madarasa 514.
Amesema katika sekta ya Elimu aliwafuta machozi wazazi kwa kufuta ada ya kidato cha 5 na 6 ili watoto wa maskini na wa kawaida watimize ndoto zao bila vikwazo huku ambapo pia kiasi cha sh. Bilioni 1 na Milioni 600 kilitolewa kwa ajili ya kulipa ada ya wanafunzi pamoja na posho kwa watumishi jambo ambalo halikuwepo huku shule 12 zenye adhi zikijengwa kwa sh. Bilioni 8.
Chalamila amempongeza wazo la Rais Samia kuamua kujengwa tawi la Chuo kikuu Cha Dar es Salaam Mkoani humo ambacho ujenzi wake utaanza Juni mosi 2023 huku ombi la mkuu huyo wa Mkoa kwa Rais Samia likiwa ni kufunguliwa kwa vyuo vinavyomilikiwa na Kanisa la KKKT na Roman Catholic vilivyofungiwa ili Mkoa huo uendelee kuwaka kiuchumi.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika sekta ya afya zimeletwa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga hospitali za wilaya katika kila Halmashauri ambapo zaidi ya sh. Bilioni 40 ziligawanyika katika sekta ya afya ikiwemo kuwajali wagonjwa wenye matatizo ya figo kwa kufunga mitambo ya usafishaji figo na kuwaondolea adha wanakagera waliokuwa wakifuata huduma hiyo Mkoani Mwanza.
Ametanabaisha pia katika Miradi mingine iliyouheshimisha Mkoa huo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Barabara, miradi ya maji, Umeme ambapo sh. Bilioni 10 zilitolewa kwa ajili ya miradi ya pembezoni mwa miji, mradi wa Rusumo wa kuzalisha megawati 80 wenye takribani dola 340 kwa ushirikiano wa Rwanda, Burundi na Tanzania unaolenga kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Toba Nguvila amempongeza Rais Dkt Samia katika kuhakikisha anaimalisha misingi, utu, usawa na uongozi bora uliodumisha amani umoja na mshikamano wa Taifa.
Nguvila amempongeza Rais Samia kwa kuleta mageuzi ya kilimo, mifugo uvuvi, ajira.
"Ni jukumu letu Wana Kagera na Watanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea ili aendelee kuliongoza taifa bila vikwazo.
Hata hiyo nao baadhi ya Wananchi Mkoani Kagera akiwemo Goleth Andrea Lucia Seba na Charles Gabone wamepongeza Rais Samia kwa kuonesha jitihadi hizo kubwa zilizoufanya Mkoa huo kuonekana kupaa zaidi katika uboreshaji wa sekta mbali mbali huku akiendelea kuwajali bila ubaguzi.
No comments:
Post a Comment