HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 09, 2023

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAWAFIKIA WANAWAKE WENYE UHITAJI HOSPITALI YA OCEAN ROAD

Meneja Mawasiliano na Uhusiano Tanzanian Commercial Bank (TCB), Gloria Mutta (watatu kulia)  akikabidhi misaada wa vitu mbalimbali kwa  Afisa Ustawi wa jamii wa Hospitali ya Ocean Road Cancer Institute (ORCI) Devotha Kibanga Kwaajili ya kusaidia wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusherehekea Siku ya Wanawake duniani inayofanyika Machi 8 ya kila mwaka, wengine pichani ni wafanyakazi wa hospital hiyo.


Na Mwandishi Wetu


Katika kusherehekea sikukuu ya mwanamke duniani, Tanzania Commercial Bank (TCB) imeendelea kuwa karibu na wateja wake katika kuzingatia usawa wa kijinsia kwa maisha endelevu. 

Tanzania Commercial Bank (TCB) imetumia sikukuu hiyo kuwakumbuka na kuwatembelea wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Ocen Road na kutoa misaada mbalimbali.

Akizungumza wakati alipotembelea wagonjwa hao Meneja mawasiliano na uhusiano wa Benki hiyo Bi. Gloria Mutta ameeleza kuwa "Tanzania Commercial Bank(TCB) imeendelea kuwa karibu na jamii kwa kutoa misaada mbalimbali hususani kwa wenye mahitaji maalum".

Ameeleza kuwa " Tanzania Commercial Bank (TCB) imetambua mchango wa mwanamke katika kuleta maendeleo"

Aliwahamasisha wanawake hao kuendelea kuiamini na kuitumia Benki hiyo kwani tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali pale tunapohitajika.

mutta aliongeza kuwa benki ya TCB  inatoa huduma nchi nzima ina matawi ambayo yanafanya kazi masaa 24 yote hayo ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma  muda wowote.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Ocean Road Cancer Institute (ORCI) Devotha Kibanga ameishukuru benki hiyo na kusema kuwa imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada kwa jamii inayotuzunguka hususani sekta ya afya.

 


No comments:

Post a Comment

Pages