HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 09, 2023

SIMBA QUEENS, JKT QUEENS HAPATOSHI MEJA ISAMUHYO

Na John Richard Marwa

Mabingwa watetezi Ligi Kuu Soka la Wanawake Tanzania Bara Serengeti Lite Women's Premier League (SWPL) Simba Queens leo wanashuka dimbani Meja Generali Isamuhyo kuwavaa wenyeji wao JKT Queens mchezo wa raundi ya 10 mzunguko wa pili wa msimu huu 2022/23.

JKT Queens wanawaalika Simba Queens ambayo ndiyo kinara kwenye msimamo akiwa na pointi 22 katika michezo tisa iliyopita huku mzunguko wa kwanza walipata ushindj dhidi ya Simba.



JKT Queens msimu huu wamekuwa na kiwango bora wakiwa hawajapoteza mchezo licha ya kukaa nafasi ya pili wakiwa wamepata sare tatu huku Simba wakipotez moja na sare moja.

Wakati Simba Queens na JKT Queens wakiumana leo Ligi hiyo mzunguko wa pili ulianza jana kwa michezo miwili kupigwa ambapo Ceasia Queens waliichapa Alliance Girls mabao (4-3) mchezo mwingine Baobab Queens waliichakaza Amani Queens mabao (3-0).

Sambamba na mchezo wa JKT Queens dhidi ya Simba Queens leo Mkwawa Queens wanawaalika The Tiger Queens, Fountain Gate Princess wakioneshana umwamba na Yanga Princess katika dimba la Jamhuri jijini Dodoma mechi zote zikitarajiwa kulindima majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Pages