HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 10, 2023

BALEKE NI HABARI NYINGINE

Na John Richard Marwa

Jean Otos Baleke, the Monster' mshambuliaji anayetisha kama jinamizi ameendeleza umwamba wa kuzifumania nyavu za wapinzani jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL dhidi ya Ihefu FC katika Dimba la Highland Estate jijini Mbeya.


Baleke ameiongoza Simba kuondoka na pointi tatu muhimu dhidi ya Ihefu amabo walikuwa wamesimika ugumu kwa timu pinzani hasa vigogo kuondoka na pointi tatu katika Dimba lao.

Ulikuwa mchezo mgumu kwa timu zote mbili kuonyeshana umahili mara baada ya siku tatu zilizopita Ihefu kuchezea kipigo kizito kutoka kwa Mnyama katika mchezo wa hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Azam Sports Federation Cup ASFC cha mabao (5-1).


Ushindi huo kwa Simba unawafanya kufikisha pointi 60 nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga SC ambao wana alama 65 kileleni mwa msimamo.

Baleke amefikisha mabao saba kwenye Ligi Kuu akiwa amejiunga na Simba dirisha dogo la usajili Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe.

Baleke tangu ajiunge na Simba mwezi Januari amecheza michezo 14 mabao 14 wastani wa bao moja katika kila mchezo aliocheza. Amefunga mabao saba Ligi Kuu, mabao manne ASFC na mabao matatu Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.

Lakini pia Baleke ndio mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi tangu mwaka huu kuanza akiwa ameweka kama 14  kwa nyota wa klabu za Ligi Kuu katika mashindano yote.

Simba waliingia kwenye mchezo huo wakiwa wanawakosa wachezaji wao nyota zaidi ya 10 huku ambao wamekuwa wakikosa nafasi wakipewa nafasi na kufanya vizuri kuiwezesha Simba kushinda katika Uwanja mgumu msimu huu kwa vigogo kuondoka na pointi tatu.

Kituo kinachofuata kwa Mnyama ni Kariakoo Derby April 16 wakiwaalika Yanga SC katika Dimba la Benjamin Mkapa kuanzia majira ya saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.


No comments:

Post a Comment

Pages