Na Victor Masangu, Kibaha
KAMPUNI
ya Kyem General Supplies Limited ya Kibaha Mailimoja
inayojishughulisha na masuala ya uuzaji na usambazaji wa vyuma
chakavu pamoja na vifaa vya ujenzi imetoa msaada wa vyakula mbalimbali
kwa watoto yatima wa kituo cha Buloma Foundation kilichopo Kata ya Sofu
katika Halmashauri ya Mji Kibaha.
Msaada
uliotolewa ni pamoja na mchele kilo 100,unga kilo 100, sukari ,mafuta
ya kupikia,sabuni na Mbuzi mmoja ambapo lengo la msaada huo ni kusaidia
watoto hao katika Sikukuu ya Pasaka.
Mkurugenzi
wa kampuni hiyo Josephu Mwakasyuka ,amekabidhi msaada huo leo katika
hafla fupi iliyofanyika katika kituo hicho huku akisema kampuni
itaendelea kutoa misaada hiyo katika makundi mbalimbali ya jamii
inayoishi katika mazingira magumu.
Mwakasyuka,
amesema kuwa kampuni ya Kyem inatambua kuwa watoto yatima ni jamii
inayopaswa kuishi kama binadamu wengine hivyo lazima wasaidiwe katika
mahitaji yao ya kila siku.
"Leo
tumeona tuje kuwaona watoto yatima wa kituo hiki cha Buloma na
tumewaletea vyakula mbalimbali kama vile mchele,unga,sukari,sabuni na
Mbuzi mmoja ili kwa pamoja viwasaidie katika sikukuu ya Pasaka ",
amesema Mwakasyuka.
Aidha,
Mwakasyuka amesema kampuni imeweka mipango endelevu ya kusaidia yatima
pamoja na jamii inayoishi katika mazingira magumu kama vile
wajane,Walemavu na wazee bila kuangalia kabila wala dini.
Hatahivyo,
Mwakasyuka amewaomba wadau wengine kujitokeza katika kusaidia watoto
yatima waliopo katika kituo hicho na hata jamii nyingine inayoishi
katika mazingira magumu kwakuwa na wao wanamahitaji sawa na binadamu
wengine.
Kwa upande wake
msimamizi wa kituo hicho Baraka Peter, ameishukuru kampuni ya Kyem
General Supplies kwa msaada huo kwani kiwango cha msaada walichotoa ni
kikubwa na kitaweza kuwasaidia mwezi mzima.
Peter,amesema
kituo hicho kwasasa kina watoto 46 ambapo kati yao wakiume ni 24 na
wakike 22 nakusema wengi wao wanasoma Shule ya awali, Msingi , Sekondari
na watoto watatu wanasoma vyuo vikuu.
"Ninatumia
fursa hii kuishukuru kampuni hii kwa msaada huu mkubwa maana
inawezekana mkaona ni kidogo lakini kwa moyo wa dhati mlichotoa ni
kikubwa Sana na kitawasaidia watoto hawa kupata chakula cha mwezi
mzima", amesema Peter
Hatahivyo
, baadhi ya watoto yatima wa kituo hicho akiwemo Lilian Masawe na
Yohana Almasi wameishukuru kampuni hiyo kwa hatua kubwa ya kuwakumbuka
katika sikukuu ya Pasaka na kuomba wasichoke kuisaidia kwakuwa
changamoto zao ni nyingi.
No comments:
Post a Comment