MAMLAKA
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua kampeni ya kuongeza uelewa kwa
umma kuhusu huduma za posta na usafirishaji wa mizigo kwa leseni na
umuhimu wake katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA, Dk. Jabiri Bakari, amesema kampeni hiyo inalenga
kukabiliana na changamoto zinazokabili watumiaji wa huduma za
usafirishaji wa vipeto na vifurushi.
Alifafanua
kuwa leseni kwa watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na vipeto
zinaongeza uwajibikaji wa watoa huduma kwa wananchi wanaowahudumia.
Kampeni
hiyo ya elimu kwa umma inalenga kuwahamasisha wananchi kutumia watoa
huduma za usafirishaji wa vifurushi walioidhinishwa na kusajiliwa rasmi,
ambazo zina ofisi zilizo rasmi, stoo za kuhifadhia vipeto na vifurushi
na rekodi nzuri ya ufanisi, usalama, na uadilifu katika utoaji huduma za
kusafirisha vipeto na vifurushi.
“Usafirishaji
wa vipeto na vifurushi unatembeza shughuli zetu za uchumi, sisi kama
mamlaka, sekta ya Posta ni sehemu ya eneo letu la usimamizi, hivyo tunao
wajibu wa kuwakumbusha watoa huduma waliopo na wanaotoa huduma za
kiposta au zinazohusiana na huduma za posta kama usafirishaji vifurushi
na vipeto kuhakikisha wanasajili huduma zao hapa TCRA na wale ambao
leseni zao zimefikia ukomo wahuishe leseni hizo.
Mkurugenzi
Mkuu Bakari aliwakumbusha watoa huduma za usafirishaji vifurushi na
vipeto yakiwemo mabasi ya abiria kwamba kufanya kazi za usafirishaji
vifurushi na vipeto bila leseni ni kutenda kinyume na utaratibu wa
sheria.
TCRA ilielekeza
kwamba wanaohitaji kusajili shughuli hizo wanaweza kutuma maombi ya
kusajiliwa kupitia lango la watoa huduma za Mawasiliano la TCRA
linalopatikana mtandaoni kupitia ukurasa wa Tanzanite Portal
unaomwezesha mwombaji kutolazimika kufika Ofisi za TCRA.
“Tumeboresha
sana huduma zetu waombaji leseni zote za mawasiliano wanaweza kupata
leseni hizo kwa njia ya lango la Tanzanite,” alisisitiza.
TCRA
inatoa leseni kwa kampuni za posta na usafirishaji wa mizigo katika
makundi sita, ikiwa ni pamoja na kimataifa, Afrika Mashariki, ndani ya
jiji, na katikati ya majiji.
Katika
kampeni ya miezi minne kuanzia mwezi Machi, watumiaji huduma za
usafirishaji vipeto na vifurushi watapewa elimu kuhusu hatari za kutumia
huduma za watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na vipeto wasio na
leseni ya TCRA; pia, watapewa Elimu kuhusu haki zao kama watumiaji
kuhakikisha zinazingatiwa.
Haki
za watumiaji wa huduma za kiposta ni pamoja na kupata taarifa kabla na
baada ya huduma kushughulikiwa kwa malalamiko na kupata nafasi ya kukata
rufani kwa Mdhibiti, miongoni mwa mengine.
Takwimu
za hivi karibuni zilizochapishwa na TCRA zinaonyesha ongezeko la
usafirishaji wa vifurushi na vipeto nchini Tanzania kutokana na ukuaji
wa biashara mtandaoni. TCRA ilisisitiza watumiaji kuhakikisha
wanajiridhisha na uhalali wa huduma za watoa huduma wanaowachagua
kuwapatia huduma.
No comments:
Post a Comment