HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 26, 2023

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa Jukwaa la 7 la Uongozi Afrika jijini Accra Ghana

 

 Rais Mstaafu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana wakiongea muda mchache kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la 7 la Uongozi Afrika (7th Africa Leadership Forum 2023) linalofanyika kuanzia leo tarehe 25  hadi kesho 26 Mei 2023, jijini  Accra, Ghana.
 Rais Mstaafu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipitia hotuba yake kabla ya  ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la 7 la Uongozi Afrika (7th Africa Leadership Forum 2023) linalofanyika kuanzia leo tarehe 25  hadi kesho 26 Mei 2023, jijini  Accra, Ghana.
 Video fupi ikichezwa Mkutanoni hapo ikimuonesha Rais wa Awamu ya Tatu na aliyekuwa Mlezi Mwanzilishi wa Jukwaa la Uongozi Afrika Hayati Benjamin William Mkapa.
Rais Mstaafu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Mkutano wa Jukwaa la 7 la Uongozi Afrika (7th Africa Leadership Forum 2023) linalofanyika kuanzia leo tarehe 25  hadi kesho 26 Mei 2023, jijini  Accra, Ghana.
 
Rais Mstaafu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana (kushoto kwake) na  Mhe. Wamkele Mene, Katibu Mkuu wa  African Continental Free Trade Area (AfCFTA - wa nne toka kulia); katika picha ya pamoja na viongozi wengine Mkutano wa Jukwaa la 7 la Uongozi Afrika (7th Africa Leadership Forum 2023) linalofanyika kuanzia leo tarehe 25  hadi kesho 26 Mei 2023, jijini  Accra, Ghana.

Viongozi wengine katika picha ni  pamoja na Mhe Jenerali  Olusegun Obasanjo Rais Mstaafu wa Nigeria (kulia kwake)  Mhe. Mohamed Moncef Marzouki (wa tatu toka kulia), Rais Mstaafu wa Tunisia, Mhe. Goodluck Jonathan Rais Mstaafu wa Nigeria (wa pili kutoka kulia) Mhe.  Thomas Bon Yayi, Rais Mstaafu wa Benin (wa tatu toka kushoto) , Mhe. Ernest Bai Koroma, Rais Mstaafu wa Sierra Leone (wa pili toka kushoto), Mhe. Hailemariam Desalegn, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia wa kwanza kulia.

Mkutano huo unaandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya Taasisi ya Uongozi ya Tanzania (Uongozi Institute) na Sekretarieti ya AfCFTA. Mhe. Kikwete ni Mlezi wa Jukwaa la Uongozi Afrika (ALF) akichukua jukumu hilo kutoka kwa aliyekuwa Mlezi mwanzilishi, Hayati Benjamin William Mkapa. Picha na Ofisi ya Rais Mstaafu


No comments:

Post a Comment

Pages