HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 26, 2023

BENKI YA CRDB ILIVYOSHIRIKI MAPOKEZI MWENGE WA UHURU ILALA


Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akiushika Mwenge wa Uhuru kabla ya haujaanza kukimbizwa katika Wilaya ya Ilala na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Meneja wa CRDB Tawi la Kariakoo, Arnold Rwamutoba, akipokea Mwenge wa Uhuru kabla haujaanza kukimbizwa katika Wilaya ya Ilala.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, akisalimiana na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd kabla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika eneo la Gerezani Ilala jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akisalimiana na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa walipokutana katika hafla ya kupokea Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika eneo la Gerezaji jijini Dr es Salaam leo Mei 26, 2023.

Meneja wa CRDB Tawi la Kariakoo, Arnold Rwamutoba, akisalimiana na Mbunge wa Ukonga, Jeery Silaa.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, akisalimiana na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea katika Wilaya ya Kigamboni.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo (katikati) akiagana na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika mapokezi ya Mwenge Wilaya ya Ilala.

Viongozi mbalimbali wakipata burudani kabla ya kuupokea Mwenge wa Uhuru eneo la Gerezani Ilala jijini Dar es Salaam.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Edward Mpogolo, baada ya kumaliza kumaliza mbio zake wilayani Kigamboni Mei 25, 2023 na kukagua miradi sita ya maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, akipokea Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili katika eneo la Gerezani Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26, 2023 ukitokea katika Wilaya ya Kigamboni.

 

No comments:

Post a Comment

Pages