HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 21, 2023

MAMA NA BABA LISHE WA MACHINGWA KOMPLEX WAPEWA MITUNGI YA GESI NA SPIKA WA BUNGE AZAN ZUNGU

Magrethy Katengu

Serikali imekuwa ikifanya jitihada za dhati kuhakikisha udhibiti wa uharibifu wa  mazingira kwa kuwapa elimu wananchi wake kutumia nishati mbadala ya kupiki ikiwemo gesi badala ya kutumia kuni na mkaa.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Naibu Spika wa Bunge la Tanzania na mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu  wakati wa anagawa mitungi ya gesi ya kupikia 40 kwa mama na baba lishe katika soko la Machinga Complex ambapo amesema kundi hilo ni muhimu sana katika jamii kwani hawana budi kujaliwa ili waondokane na matumizi ya mkaa na kuni ili kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira .

Naibu Spika amesena Ugawaji wa mitungi hiyo ni sehemu ya mitungi 200 iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa masoko ya Machinga Complex, Karume, Ilala na Mchikichini kuonesha moyo wa upendo kuwa analijali kundi hilo

  "Zoezi hilo la ugawaji wa mitungi inakwenda kusaidia  upikiaji wa gesi na ni faida nyingi ikiwemo kuokoa fedha na kuepukana na madhara ya kiafya ikiwemo kifua ambapo amedai kuwa mtu anayepikia kuni na mkaa kwa siku ni sawa na mtu anayevuta sigara 300 kwani moshi unaotoka jikoni anavyovuta hewa humwaathiri kidogokidogo na baadae kupata ugonjwa wa kifua kikuu"amesema Naibu Spika

Kwa upande wake Meneja wa somo la Machinga Complex Stella Mgumia amewahimza wafanyabishara wanafanya biashara ndogondogo mitungi hiyo waliyopewa waitumie kwa mlengo uliokusudiwa siyo kwenda kuuza au kupeleka majumbani mwao


Nao Mama lishe na Baba lishe mama na baba lishe katika soko la Machinga Complex Amina Masoudi na Alex Silian wameshukuru sana kupewa zawadi hiyo kutoka kwa Rai Mama Dkt Samia Suluhu Hassani kumtuma Spika na wamepokea kwa furaha isiyo kifani  Mitungi na  itaenda kuwasaidia katika shughuli zao za kila.


No comments:

Post a Comment

Pages